January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Askari Tanapa apata Tuzo Afrika

Faru akiwa kwenye hifadhi za Ngorongoro, mkoani Arusha

Spread the love

ASKARI  wa Wanyama pori wa (TANAPA), Patrick Mwita ameshinda tuzo ya kila mwaka ya Askari Bora katika ulinzi wa Faru  kwa mwaka  2015 barani Afrika zinazofahamika kama “2015 Rhino Conservation Award”. Anaandika Ferdinand Shayo, Arusha … (endelea).

Tuzo hizo zilizotolewa Jijini Johanesburg nchini Afrika Kusini 27 Julai Mwaka huu zimeiletea Tanzania heshima ya kimataifa kutokana na vigezo mbalimbali vilivyotumika ikiwemo vitendo vya kijasiri na kishujaa.

Afisa Mahusiano wa TANAPA, Pascal Shelutete amesema kuwa Patrick Mwita ni askari mwenye uwezo wa kuwatambua faru asilimia zaidi ya 90% ya Faru walioko Serengeti kwa kutumia alama zao za asili alishiriki kupambana na majangili wenye silaha nzito.

IMG_20150731_115311

Mshindi wa Tuzo hizo Patrick Mwita amesema kuwa licha ya kuliletea taifa heshima kupitia tuzo hizo bado Tanzania inakabiliwa na changamoto ya ujangili hivyo jitihada zaidi zinahitajika ili kuhakikisha kuwa wanyama wanalindwa kwa faida ya taifa ,vizazi  vijavyo na dunia kwa ujumla.

Kaimu Mhifadhi wa TANAPA , Mtango Mtahiko amesema kuwa tuzo hiyo ni chachu ya kuongeza ulinzi kwa wanyamapori na kutoa hamasa kwa Wananchi kushiriki katika kulinda uhifadhi usipotee.

Faru ni moja kati ya wanyama pori ambao wako hatarini kutoweka kutokana na vitendo vya ujangili, serikali, mashirika binafsi na wananchi wana jukumu kubwa la kulinda urithi huu wa asili ambao tunu kwa taifa na dunia nzima.

error: Content is protected !!