Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Askari polisi 7 wa Tanzania walioingia Malawi watimuliwa
Habari Mchanganyiko

Askari polisi 7 wa Tanzania walioingia Malawi watimuliwa

Spread the love

 

ASKARI saba wa Jeshi la Polisi Tanzania wamefukuzwa kazi baada ya kuvuka mpaka na kuingia nchini Malawi kinyume cha utaratibu wa jeshi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Songwe … (endelea).

Askari hao ni wa Wilaya ya Ileje Mkoa wa Songwe ambao tarehe 15 Septemba 2021, wakiwa wamevalia sare za jeshi hilo waliingia Malawi wakidaiwa kufukuzia magendo.

Wakiwa huko, wananchi wa Malawi waliwavamia na kuanza kuwapiga na kuharibu gari la polisi.

https://youtu.be/cPCxiUNTdHk

Leo Jumanne, tarehe 21 Septemba 2021, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, ACP Janeth Magomi ametangaza kufukuzwa kazi askari hao kwa kuingia Malawi pasina kibali cha Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP).

Kamanda Janeth amewataja askari hao saba waliotimuliwa; ni PC Edward, PC Safari, PC Joseph, PC Hussein, WP Anastazia na PC Jumanne ambaye alikuwa dereva.

Amesema, askari hao wanaweza kufuata utaratibu na kukata rufaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mawakili waiburuza mahakamani TLS, EALS

Spread the love  WAKILI Hekima Mwasipu na wenzake wawili, wamefungua kesi katika...

Habari Mchanganyiko

Uvuvi bahari kuu wapaisha pato la Taifa

Spread the love  SERIKALI imesema uvuvi wa bahari kuu umeliingizia Taifa pato...

Habari Mchanganyiko

DPP aweka pingamizi kesi ya ‘watu wasiojulikana’

Spread the love  MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), ameweka pingamizi dhidi ya...

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

error: Content is protected !!