Monday , 27 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Askari mwingine wa Tanzania afariki DR Congo
Habari Mchanganyiko

Askari mwingine wa Tanzania afariki DR Congo

Spread the love

WALINDA amani saba wa Umoja wa Mataifa akiwemo Mtanzania mmoja na wanajeshi sita wa Malawi wamepoteza maisha katika operesheni ya pamoja iliyofanywa na kikosi chake na Jeshi la DR Congo dhidi ya kundi la waasi la ADF. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Kwa mujibu wa Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, tukio hilo limetokea hivi karibuni katika mji wa Beni Kaskazini mwa Kivu, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo hadi sasa hakuna kundi lililobainika kutekeleza shambulio hilo.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa, kuna walinda amani kadhaa kutoka Jeshi la Congo pia wameripotiwa kuuawa au kujeruhiwa wakati askari kumi wakijeruhiwa huku mmoja akipotea kusikojulikana.

Dujarric amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ametuma salamu za rambi rambi kwa familia za walinda amani waliopoteza maisha, na kuvitaka vikundi vinavyotekeleza mapigano kusitisha kwani mapigano hayo yanaleta ugumu katika kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Mji wa Beni ulioko Kaskazini mwa Kivu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ni eneo lililoathiriwa zaidi na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Chanzo: BBC Swahili

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa  Ligi Kuu ya NBC, yaahidi maboresha zaidi

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League),...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

ElimuHabari Mchanganyiko

Rubani mtarajiwa Tusiime awashangaza wazazi

Spread the loveWAZAZI walioshiriki siku ya taaluma na maonyesho ya shule ya...

Habari Mchanganyiko

Wanne wadakwa kwa kusafirisha punda 46 nje ya nchi

Spread the loveJeshi la Polisi kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa...

error: Content is protected !!