Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Askari magereza mbaroni tuhuma za kubaka, kujiua
Habari Mchanganyiko

Askari magereza mbaroni tuhuma za kubaka, kujiua

Spread the love

 

JESHI la Polisi Mkoa wa Ilala, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linamshikilia Said Hassan Said (26) ambaye ni askari Magereza, Mkazi wa Ukonga kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti msichana mwenye umri wa miaka 29. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa, tarehe 3 Septemba 2021, Kamanda wa Polisi wa Ilala, Debora Magiligimba amesema, tukio hilo lilitokea 1 Septemba 2021, saa 5:30 usiku katika barabara ya madafu Ukonga.

Amesema, mtuhumiwa huyo ambaye ni askari wa Jeshi la Maagereza mwenye namba B 9780 WDR Said Hassan akiwa na mwenzake ambaye bado hajakamatwa walimkamata kwa nguvu msichana huyo na kumuingiza kwenye gari dogo kisha kuondoka naye hadi nyumba moja iliyopo karibu na kambi ya KMKM Ukonga Magereza na kuanza kumbaka na kumlawiti kwa zamu.

“Baada ya kumaliza kumbaka na kumlawiti, watuhumiwa hao waliendelea kumfanyia vitendo vya ukatili wa kijinsia na kumsababishia majeraha makubwa na maumivu makali katika sehehmu zake za siri,” amesema Kamanda Debora.

Aidha, amesema baada ya mtuhumiwa kugundua kuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa tukio baya alilolifanya na mwenzake, tarehe 2 Septemba 2021 alijaribu kujiua kwa kujinyonga na kuacha ujumbe wa maandishi kwa mkuu wake wa kazi na askari wenzake kuwa “mnisamehe bure kwa uamuzi wangu niliochukua kwa tukio nililolifanya nitaonekana nimekufa kizembe.”

Kamanda huyo amesema, kabla hajafanikisha azma yake ya kujitoa uhai alikamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi.

Amesema, wanaendelea na msako mkali kwa mtuhumiwa mwenzake aliyekimbia baada ya tukio hilo baya na linamtaka ajisalimishe haraka iwezekanavyo katika kituo chochote cha Polisi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

Habari Mchanganyiko

Uholanzi wampongeza Rais Samia kuimarisha vyombo vya habari, demokrasia

Spread the love  UBALOZI wa Uholanzi nchini Tanzania, umempongeza Rais Samia Suluhu...

error: Content is protected !!