January 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Askari Magereza 16 wapata makazi bora

Moja ya jengo jipya la Magereza

Spread the love

FAMILIA 16 za askari Magereza kati ya 63 katika Manispaa ya Iringa, zimepata makazi bora baada ya kukamilika kwa jengo la ghorofa tatu ambalo ni kati ya manne yanayohitajika. Anaandika Edson Kamukara … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea miradi ya Magereza mkoani humo, mhandisi wa jengo hilo, Mrakibu wa Magereza, Angalipo Mwakarobo amesema kuwa zipo familia za askari 63 wanaohitaji kupatiwa makazi bora.

Amesema, “ili kuwapatia nyumba bora askari wote, tunahitaji majengo kama hili manne, lakini hadi sasa serikali imetoa fedha za kukamilisha ghorofa moja ambalo limegharimu sh. 1.1 bilioni”.

Kwamba gharama za awali za ujenzi huo ulioanza tangu mwaka 2007, zilikuwa ni sh. milioni 900.8, lakini kadiri fedha zilivyocheleweshwa kutoka serikali, gharama hizo zilipanda na kufikia sh. bilioni 1.1 mwaka 2012 ujenzi ulipokamilika.

“Tunaiomba serikali itupatie nyongeza ya majengo matatu kama tulivyoomba ili ujenzi uanze na kukamilika, kusudi askari wetu waondokane na kadhia ya kukaa kwenye makazi yanayowashushia hadhi.

“Itakuwa jambo la ajabu kama serikali itaboresha magereza ili wahalifu wakae mahala pazuri halafu askari wanaolinda wafungwa wanakaa kwenye makazi duni, ambayo hata ndugu zao wakiwatembelea wanaona aibu,” amesema.

error: Content is protected !!