May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Askari JWTZ aeleza alivyomripoti Mbowe kwa DCI na ACP Kingai

Spread the love

 

SHAHIDI wa 12 wa Jamhuri, katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, ASKARI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Denis Urio, amedai alimripoti mwanasiasa huyo kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Boaz, kuhusu mipango yake ya kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar ea Salaam … (endelea).

Luteni Urio ametoa madai hayo leo Jumatano, tarehe 26 Januari 2022, akiongozwa kutoa ushahidi wake na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Abdallah Chavula, kwenye Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam, mbele ya Jaji Joachim Tiganga.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine kwenye kesi hiyo yenye mashtaka sita ya ugaidi, ni waliokuwa makomandoo wa JWTZ, Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Luteni Urio amedai kuwa, alimripoti Mbowe kwa DCI Boaz akiwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha (RCO), ACP Ramadhan Kingai, Julai 2020, baada ya mwanasiasa huyokumuomba amtafutie makomandoo wa mufanikisha harakati zake za kuchukua dola.

Kwa kuandaa maandamano yasiyo na kikomo, kuchoma vituo vya mafuta na mikusanyiko ya watu, pamoja na kudhuru viongozi wa Serikali.

Yafuatayo ni mahojiano kati ya Luteni Urio na Wakili Chavula;

Chavula: Shahidi baada ya kumpa maneno hayo nini kilitokea?

Shahidi: Wakati naendelea kumpa maneno hayo alikuwa anafanya mawasiliano kumpigia mtu aje kwenye ofisi yake mimi nilikaa hapo akaja, akamsalimia Afande DCI.

Chavula: Mawasiliano gani aliyafanya?

Shahidi: Alikuwa anapiga simu

Chavula: Kwa hiyo alipopiga simu nini kilitokea?

Shahidi: Baaada ya hapo aliingia mtu katika ofisi yake

Chavula: Ilipita muda gani yule mtu kuingia?

Shahidi: Kama dakika 10 hivi

Chavula: Tuambie yule mtu aliyeingia pale mkawa mmekaa mnatazamana, siku ile ilikuwa mara yako ya ngapi kuonana naye?

Shahidi: Mara yangu ya kwanza

Chavula: Iambie mahakama huyo mtu alivyoingia mkawa mmekaa mnatazamana nini kielendela?

Shahidi: Nakumbuka Afande DCI akanitambulisha kwake kuwa anaitwa ACP  Ramadhan Kingai

Chavula: Baada ya utambulisho huo?

Shahidi: Ndiyo DCI Robert Boaz akanitaka nianze tena upya kusimulia hizo taarifa

Chavula: Ianbie mahakama uliwaleza nini?

Shahidi: Niliwaeleza kwamba jana nilipigiwa simu na Mbowe akinitaka nikutane naye maeneo ya Mikocheni na kwamba nilikutana naye maeneo ya Mikocheni, nilifanya hivyo.

Mbowe akanieleza haya yafuatayo kwamba, mwaka huu wa uchaguzi mkuu wamedhamiria kuchukua dola kwa namna yoyote ile. Na kwa sababu hii nafahamiana naye kwa muda mrefu, wakichukua dola nitapewa cheo kikubwa jeshini.

Hivyo akaniomba sasa nimtafutie askari waliostaafu au waliofukuzwa kazi jeshini ambao wamefanya mafunzo maalumu akiwa na maana makomando, ili aama

batane nao katika harakati hizo za kuchukua dola, kwa  kufanya matukio ya kuifanya nchi isiwe na amani ns isitawalike.

Kwa kufanya matendo  yafuatayo ili kufanya nchi isitawalike, watalipua vituo vya mafuta katika majiji matano makubwa,  ambayo ni Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza, Arusha na Moshi kilimanjaro.

Kukata miti na kupanga magogo barabarani, matendo hayo yataanzisha taharuki kwa wananchi na kuonesha Serikali imeshindwa kulinda wananchi wake, ili wao watangaze maandamano nchi nzima.

Pia nikaendelea kumueleza Kingai na DCI Boaz kwanba wamepanga kuwashambulia viongozi wa kiserikali ambao ni kikwazo kwa vyama vya upinzani na ndiyo ilikuwa taarifa yangu niliyompa DCI Boaz

Chavula: Nini kilichoendelea?

Shahidi: DCI alimuita Kingai akamfuata pale alipokaa, wakawa wanaketi wao wawili, mimi sijui walikuwa wanazungumza kitu gani.

Baada ya muda kama dakika 10 DCI akamtaka Kingai anipe namba zake za simu, kwa maana ya mawasiliano na mimi nimpe mawasiliano yangu

Boaz akanipa maelekezo niendelee na huo utaratibu ambao Mbowe anataka nifanye kuwatafuta hao watu anaotaka na kila hatua niwe naripoti kwa ACP  Kingai

Chavula: Alikupa maelekezo gani?

Shahidi: Nimsikilize Mbowe anataka makomandoo wangapi na kunitaka kutoa kila ripoti kwa Kingai

Chavula: Alikuambia uwape malekezo gani hao watu uliokuwa unawatafuta?

Shahidi: Aliniambia nikiwapata hao watu nimueleze chochote

Chavula: Baada ya kuwa umepewa hayo maelekezo nini kilichofuata?

Shahidi: Niliachana na Afande DCI  nikaendelea na shughuli zangu lakini wakati huo sababu tayari alinipa amri niendelee kwa utaratibu huo, nikaanza mchakato wa kuwatafuta watu.

Nilianza kumtafuta mtu anayeitwa Moses Lijenje, naye alikuwa askari aliyefukuzwa jeshi 2008 kwa utovu wa nidhamu. Nilifahamiana naye toka 2003 mpaka 2008.

Chavula: Aliuwa anafanya kazi gani?

Shahidi: Alikuwa katika kampuni ya Yapi inayotengeneza reli

Chavula: Ulitamfuta kwa njia gani?

Shahidi: Nilimtafuta kwa njia ya simu, nilipompata nikamwambia kuna kazi ya ulinzi ya Mbowe, unaweza kufanya kazi hiyo, akaniambia anaweza kufanya kazi hiyo kwa kuwa amepunguzwa kazi kwa muda kwa sababu ya korona kwa hiyo yuko tayari. Nikamwambia subiri Mbowe akiwahitaji nitamjulisha.

Chavula: Nani mwingine ulifanikiwa kumpata?

Shahidi: Nikamtafuta Halfan Hassan Bwire kwa njia ya simu, alikuwa hapatikani nikamtumia meseji  kwa njia ya mesenja.

Chavula: Iambie mahakama  naye ulipompata ulimueleza nini?

Shahidi: Nikamueleza Mbowe anahitaji walinzi, je uko tayari akaniambia yuko tayari kufanya kazi

Chavula: Yeye alikuwa wapi?

Shahidi: Alikuwa yupo anafanya kazi ya kusafirisha magari kwenda Tunduma

Chavula: Hayo magaro kutokea wapi?

Shahidi: Sikujua yanatokea wapi

Chavula: Baada ya kuwa amekukubalia wewe ulimpa maelekezo gani?

Shahidi: Nilimwambia subiri muda atakapohitajika na Mbowe nitamjulisha

Chavula: Baada ya kumpata mtu wa pili ulifanya nini?

Shahidi: Nilimsubiri wmenye uhitaji kama yuko serious atanitafuta tena

Chavula: Nini kilitokea baina yako wewe na Mbowe baada ya kuwa umepata watu wawili?

Shahidi: Nilitulia baada ya siku chache Mbowe akanipigia simu akaniambia home boy mbona mpaka sasa hivi kimya, wale watu mbona hukunitumia? Hapo ndio nikajua yuko serious nikamwambia watu wako ni wa kutumia nauli ili kuwamobilize kuja kwenye eneo alipo.

Akaniuliza kianzio shilingi ngapi, nikamwambia laki tano

Chavula: Iambie mahakama hayo amqaisliano mlikwua mnafanaya kwa niia gani?

Shahidi: Mawasiliano makubwa ilikuwa kwa njia ya Telegram, alikuwa anapiga simu ya voice kupitia Telegram, sababu nilikuwa nikimpigia normal call hapokei hata siku mojs otherwise atumie simu ya mtu lakini sio simu yake

Chavula: Ilikuwa siku gani?

Shahidi: Tarehe 20 Julai 2020, tuliwasiliana kwa njia ya voice ns meseji kwenye Telegram

Chavula: Iambie mahakama ulipomwambia kwamba inahitajika Sh. 500,000, nini kilitokea?

Shahidi: Aliniambia nimpe namba ya kutuma hiyo laki tano, nikamtumia namba yangu ya Airtel 0787555200

Chavula: Tuambie ulivyomtumia hiyo namna nini kilitokea?

Shahidi: Alinitumia shilingi  laki tabo cash kwa njia ya simu kwenye namba yangu ya Airtel kupitia mtandao wake wa Tigo 0719933386

Chavula: Alikutumia tarehe ngapi?

Shahidi: 20 Julai 2020

Chavula: Pesa hiyo ilikuwa kwa malengo gani?

Shahidi: Pesa hiyo ilikuwa kwa malengo ya kuwapeleka watu kwenda kufanya uhalifu

Chavula: Baada ya hapo ulimwambia nini ACP Kingai?

Shahidi: Nikamuarifu  keamba Mbowe amenitumia kiasi hicho cha pesa na walishapatikana watu wawili  akaniambia sawa we endelea watumie hela waende walikotaka waende

Nikampigia Lijenje nikamwambia kazi tayari aje Morogoro. Nikampigia na Bwire akasema naye anakuja. Nikakutana nao Msamvu Terminal Morogoro.

Chavula: Ieleze mahakama hizo fedha ulizotumiwa ulizifanyia nini?

Shahidi: Nilizitoa hazikutoka cash laki tano, zilitoka 499,000

Chavula: Iambie mahakama wale watu ulivyoonana nao baada ya Bwire na Lijenje, nini kileindelea?

Shahidi: Niliwaambia kuna kazi ya ulinzi kwa Mbowe, kama nilivyowaeleza mwanzo, wakasema wako tayari. Nikawaambia mna kiapo ninyi ni askari kile kiapo chenu hakijavunjwa.

Chavula: Tuambie endelea kutueleza

Shahidi: Nikawaambia mnaenda kufanya kazi kwa Mbowe, lakini mnapokuwa kwa mwajiri wenu huyo mnakoenda, matukio yoyote, matendo yoyote ya kihalifu mtakayoona yanafanyika huko muwe mnaniambia.

Mipango ya uhalifu inayofanyika muwe mnanipa taarifa, huyo ni Bwire akasema hamna shida. Nikatoa Sh. 300,000 kutoka hela za Mbowe nikawapa, nikamwambia Mbowe vijana wako tayari.

Chavula: Hayo mawasiliano mliyokuwa mnafanya, mlikuwa mnatumia aina gani ya mtandao?

Shahidi: Mfumo wa Telegram

Chavula: Baada ya kufika Dar es Salaam ulimwmabia nini ACP Kingai?

Shahidi: Walipofika Dar es Salaam nikaripoti kwa Kingai, Moses Lijenje na Bwire wako kwa Mbowe.

Chavula: Tuambie umepeleka watu wawili, umetoa taarifa kwa Kingai, nini kilichofuata baada ya hapo?

Shahidi: Mbowe akaniambia bado wengine wawili

Chavula: Baada ya kueleza hivyo wewe ulifanyaje?

Shahidi:Nikaanza kutafuta wengine wawili, Adam Lasekwa na Halfan Bwire. Adam Kasekwa alipatikana kwa njia ya simu, nilimpigia simu  Ling’wenya, alipokuja akamtafuta mwenzake Adam Kasekwa.

Chavula: Iambie mahakama ulikutana nao wapi hawa wawili?

Shahidi: Nilikutana nao Msamvu Stendi ya Morogoro mjini

Chavula: Tuambie ulipokutana ulizungumza nao kuhusiana na nini na mlikubaliana nini?

Shahidi: Tulipokutana nao nikawaambia Mbowe anataka askari waliofanya mafunzo maalum kwa ajili ya ulinzi, wakaniambia wako tayari. Laki 199,000 iliyobakia nikawapa.

Nikawaambia mnaenda kufanya ulinzi mnakiapo cha uaskari, chochote mtakachokiona kipo tofauti muwe mnaniambia. Katika weledi askari hawezi kuwa raia, lakini raia anaweza kuwa askari hivyo basi chochote kutakachotokea niambie.

Nikampigia Mbowe nikamwambia hao watu wawili wako tayari. Akanitumia Sh. 165,000 kwa ajili ya nauli yao kutoka Morgoro kwend Dar es Salaam.

Chavula: Alikutumia kwa njia ipi na namba gani?

Shahidi: Alituma kwa njia ya wakala

Chavula: Nini kilipeleka ukatumiwa kupitia wakalaa na si simu yake?

Shahidi: Kilichopelekea kunitumia kupitia wakala nahisi alimpa mtu kwenda kunitumia, kwenye namba yangu ya simu

Chavula: Ulijuaje kama imetoka kwake?

Shahidi: Alinitumia meseji kwenye Telegram, akaniuliza nimekutumia umezipata, nikamjibu nimezipata. Niliwapa Adam na Ling’wenya kwa usafiri kuja Dar es Salaam

Chavula: Baada ya kuwapatia pesa nini kiliendelea?

Shahidi: Wakanza safari kutoka Morogoro kwenda Dar es Salaam

Shahidi: Walipoanza hiyo safari wewe ukafanya nini?

Shahidi: Walipoanza safari nikam-brief Mbowe vijana hao wanakuja, akamwambia Bwire awasiliane nao

Chavula: Wakati unatafuta vijana unawapa unawambia wnaenda kufanya kazi ya ulinzi kwa nini  ulifanya hivyo?

Shahidi: Nilifanya hivyo kwa sababu ya kiusalama

Chavula: Unaamanisha nini?

Shahidi: Namaanisha kwamba, hawa ni askari waliofukuzwa kazi lakini haujawatoa uaskari wao, lakini bado wana viapo vyao.

Viapo havijatenguliwa, ukiwaambia wanaenda kufanya uhalifu utaharibu unachofanya, ndiyo maana nikawaambia mkiona matukio ya kihalifu mniambie, ningewaambia wangeharibu wasingeweza kujizuia kuongea

Walivyoondoka akaacha mawasiliano na mimi, akaniona useless, nikimpigia hapokei nikamtumia ujumbe hakujibu, sikujua nini kinachoendelea

Chavula: Mawasiliano yako wewe na Kasekwa baada ya kuwapa fedha wakaenda Dar es Salaam yalikuwaje?

Shahidi: Hatukuwahi kuwa na mawasiliano sababu sikuwahi kuwa na namba yake

Baada ya kufika nikaona kimya nikawa nampigia Bwire simu hapokei, anakwambia niko busy nilikwua nawasiliana kwa njia ya WhatsApp na Ling’wenya, nikitaka kujua kuna kitu gani kinachoendelea huko. Kuna mapya gani mmeambiwa, nini mnachofanya akaniambia boss katuambia atatuajiri na kuwalipa mshahara kila mwisho wa mwezi

Chavula: Boss wao ni nani?

Shahidi: Freeman Aikael Mbowe

Chavula: Mawasiliano yako na Ling’wenya yakaishia wapi?

Shahidi: Baada ya kumuuliza kitu kingine, ananijibu kitu kingine yakaishia hapo

Chavula: Tueleze mawasiliano yako wewe na Bwire yalikuwaje?

Shahidi: Mara nyingi alikuwa yuko busy na yeye nilikuwa nampigia kila siku kutaka kujua wako wapi na wanafanya nini.

Nakumbuka nilimpigia tarehe za mwisho za Julai, Bwire akaniambia tuko Dar es Salaam lakini tutakwenda Moshi. Nikamwmabia kazi gani hiyo, akaniambia ya ulinzi tuko Moshi hapa nitakwambia baadae.

Baada ya kuona kimya tarehe 4 Agoati 2020 , nikampigia simu tukasalimiana akaniambia bro samahani sijakutafuta kama ulivyonielekeza kwa sababu tumekenguka ulivyotuambia. Samahani nimepitia yale uliyoniambia sijayafanya.

Kazi uliyotuambia tunakuja kuifanya ya ulinzi wa Mbowe imebadilika sio hiyo. Kwmaba Mbowe ametushawishi kufanya kazi nyingine ambayo hivi sasa tunavyoongea wale madogo ina maana Moses Lijenje, Kasekwa na Ling’wenya wako Moshi sasa hivi.

Wamepewa kazi ya kumshambulia Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na kabka ya tarehe 7 Agosti 2020, wanatakiwa wawe wameshamaliza kazi hiyo warudi Dar es Salaam, kwa sababu tarehe 12 Agosti 2020 kuna kazi nyingine wanayokuja kuifanya Dar es Salaam. Mwisho wa taarifa niliyopokea kutoka kwa Bwire.

Chavula: Baada ya yeye kukupa taarifa hiyo akamueleza nini?

Shahidi: Baada ya kunipa taarifa hiyo nikamwambia aendelee kuwasiliana na mimi.

Chavula: Baada ya Bwire kukupa taarifa hiyo ulifanya nini?

Shahidi: Baada ya kuipokea taarifa hiyo papo hapo nikampigia ACP Kingai simu, nikamwambia taarifa nilizozipata muda huu ninaokupigia simu, Moses, Kasekwa na  Ling’wenya wako Moshi kutekeleza jukumu la Mbowe la kumshambulia Mkuu wa Wilaya ya Hai.

Hivi sasa Moses Kasekwa Ling’wenya wanafanya ufuatiliaji maeneo ambayo Lengai Ole Sabaya anayopenda kutembelea kati ya maeneo ya Moshi na Jiji la Arusha, mwisho wa taarufa yangu kwa ACP Ramadhan Kingai.

Chavula: Hii taarifa ya kwamba wanatembelea maeneo ambayo huyu Ole Sabaya anapenda kuhudhuria uliitoa wapi?

Shahidi: Tarege 4 nilivyoongea na Bwire, ndiyo nilipewa taarifa hizo

Chavula: Baada ya kuwa umemaliza kutoa taarifa kwa Kingai ulifanya nini?

Shahidi: Akasema nashukuru kwa taarifa nitafuatilia. Tarehe 5 Agosti 2020 nikampigia simu Bwire akaniambia Adam na Ling’wenya wamekamatwa.

Chavula: Alikueleza Adam na  Ling’wenya wamekamatwa na kina nani?

Shahidi: Aliniambia hao madogo wamekamatwa, nikamuuliza boss wenu Mbowe anafahamu? Aliniambia anafahamu

Chavula: Baada ya kumuuliza nini kiliendelea, ama ulifanya nini?

Shahidi: Nilichukua hatua ya kumpigia Mbowe simu, hakupokea nikapiga tena hakupokea, nikapiga tena na tena hakupokea, kumbuka toka tarehe 24 Julai alikata mawasiliano na mimi baada ya kuwapokea, walivyokamatwa nikampigia simu hakupokea.

Baadae nikaja nikakuta ujumbe wake Telegram kwenye akaunti yangu, ambao ilikuwa tarehe 6 Agosti 2020.

Chavula: Ujumbe ulikuwa na maudhui gani?

Shahidi: Kwamba nimeshindwa kupokea simu ya kawaida kwa sababu dash dash (vinukta nukta aliweka) najua umenielewa, mbele akaendelea enemy…mengine nishasahu

Chavula: Iambie mahakama umeambiwa najua unanielewa wewe, ulielewa nini?

Shahidi: Siwezi kuwa na tafsiri lakini nilijua ni kwa sababu za kiusalama

Chavula: Baada ya kupoeka ujumbe nini kiliwndelea?

Shahidi: Baada ya hapo sikuhangaika naye, Bwire alinipigia simu tarehe 7, 8, 9 sikupokea

Chavula: Sababu gani ulikuwa hupokei simu za Bwire?

Shahidi: Kwa sababu tayari lengo lilikuwa limeshatimia, nilikuwa nishapata taarifa wamekamatwa sasa natafuta nini

Chavula: Nini kiliendelea?

Shahidi: Baada ya hapo nilikuwa naendelea na shughuli zangu za kawaida, tarehe 10 Agosti 2020, majira ya saa 9 saa 10 jioni  akanipigia ACP Kingai simu, akanitaka niende Makao Mkuu ya Polisi, yaliyopo Dar es Salaam maeneo ya Posta mpya.

Akaniambia kesho uende Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam, utakutana na afisa wa polisi anayeitwa Inspekta Swilla, akanitumia namba zake za simu.

Chavula: Wakati huo ulikuwa uko wapi?

Shahidi: Nilikuwepo Morogoro

Chavula: Baada ya kupewa malekezo hayo ulichukua hatua zipi?

Shahidi: Nilichukua hatua ya kusafiri kutoka Morogoro kuja Dar es Salaam, siku hiyo ya tarehe 10 Agosti 2020, ili kuonana na Inspekta Swilla kesho yake

Chavula: Tuambie hiyo siku ya tarehe 11 Agosti 2020, ulifanya nini?

Shahidi: Majira ya saa 2 nikaenda Makao Makuu ya Polisi, nikafuata taratibu za Jeshi la Polisi, nilifika mlangoni nikakuta askari wawili nikajitambulisha nikatoa kitambulisho changu nikawaambia nataka kuonana na Inspekta Swilla, nikampigia simu akaja pale chini nikapanda naye juu kwenye ofisi yake

Chavula: Mlipofika ghorofa ya nane nini kiliendelea?

Shahidi: Nilipofika nikakaa, akaniambia amepewa maelekezo anichukue maelezo ya matukio, nikamkubalia akaanza kunichukua maelezo kuhusu Freeman, Halfan Bwire na wenzie.

Akanichukua maelezo baada ya hapo nikasaini maelezo, akaniomba niwaachie simu kwa sababu ya upelelezi. Simu niliyokuwa nayo akaomba nimuachie kwa sababu ya uchunguzi wa mawasiliano tuliyokuwa tunafanya kazi yangu na Bwire pamoja na Mbowe.

Chavula: Wakati anakwambia hayo hiyo simu uliluwa unafamya mawasiliano na hao uliowataja, simu ilikuwa wapi?

Shahidi: Nikamwambia laini zangu nilizokuwa nafanya nao mawasiliano.

Chavula: Wewe ulikuwa unatumia simu ngapi kufanya nao mawasiliano?

Shahidi: Simu nne, simu ya kwanza Tecno Cammon, Tecno C9, Itel, Sumsung ya tochi

Chavula: Simu hizi ulikuwa ukitumia mitandao gani ya simu kufanya mawasiliano?

Shahidi: Nilikuwa nikitumia mtandao wa Airtel, Vodacom, Halotel, Tigo kwa Tanzania.

Chavula: Unaposema ya Tanzania una maanisha nini?

Shahidi: Kulikuwa na laini nilizokuwa natumia Sudan, MTN Sudan na Zain.

Chavula: Ulipotakiwa kuacha simu zako wewe ulifanya nini?

Shahidi: Kitu cha kwanza kwa sababu sikujua naenda kufanya nini, nilitoa Cheap ya simu ya  Voda, Tecno Cammon nikaweka kwenye Sumsung ya tochi nikaacha ile simu, nikamwambia simu nyingine nitakuletea.

Chavula: Iambie mahakama ulipomuachia ile simu yako ya Tecno ni taratibu gani zilifanyika katika kuachiana?

Shahidi: Akachukua simu, akafungua ndani aka-register IMEI namba kwenye nyaraka, akasaini na mimi nikasaini akanipa copy (nakala).

Chavula: Iambie mahakama hiyo nyaraka unayosema iliandikwa mkasainishana ukiiona kama utaweza kuitambua?

Shahidi: Naweza

Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho Alhamisi, ambapo Luteni Urio ataendelea kutoa ushahidi.

error: Content is protected !!