October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Askari 818 wahitimu, wawili watimuliwa chuo cha uhamiaji

Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji, Mrakibu Moses Lusamba

Spread the love

 

MKUU wa Chuo cha Uhamiaji, Mrakibu Moses Lusamba, amesema jumla ya askari 818 wamehitimu mafunzo ya awali ya chuo cha uhamiaji huku wawili wakishindwa kuhitimu baada ya kufukuzwa kwa utovu wa nidhamu. Anaripoti Erick Mbawala, TUDARCo … (endelea).

Amesema mafunzo hayo kozi namba 1/2022 yalifunguliwa rasmi tarehe 2 Januari, 2022 yakiwa na jumla ya Askari wanafunzi 820.

Lusamba amebainsha hayo leo Jumatatu tarehe 15 Agosti, 2022 katika hafla ya kufunga mafunzo hayo na kuwekwa jiwe la msingi wa ujenzi wa chuo hicho kilichopo Boma Kichakamiba wilayani Mkinga mkoani Tanga.

Aidha Lusamba ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan,kufuatia hatua ya serikali kujenga miundombinu ya chuo hicho.

Akitoa taarifa fupi kuhusu mafunzo ya Askari wapya waliohitimu mafunzo, Lusamba ameishukuru Serikali kwa kujenga majengo mapya pamoja na kumalizia ujenzi wa jumla ya majengo 34, ambayo bado yalikuwa hayajakamilika. “Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita imetuwezesha kujenga majengo mapya 34,” amesema.

Pia Lusamba ametaja mafanikio ambayo wameyapata tangu wafanye maboresho ya chuo hicho, ikiwemo uanzishwaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile miradi ya kufyatua tofali na kiwanda cha kuoka sambamba na kutoa mafunzo kwa zaidi ya watu 1,000.

error: Content is protected !!