Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Asimilia 79 wafeli somo la hesabu matokeo kidato cha nne
Habari Mchanganyiko

Asimilia 79 wafeli somo la hesabu matokeo kidato cha nne

Spread the love

WATAHINIWA wa shule 415,844 sawa na asilimia 79.92 ya watahiniwa 520,558  wenye matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2022 wamepata daraja F katika somo la Hesabu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Matokeo hayo ya mitihani iliyofanyika Novemba na Desemba 2022, yametangazwa leo Jumapili tarehe 29 Januari 2023 na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitahani Tanzania (NECTA), Athumani Amasi.

Somo hilo ambalo ni la lazima kwa wanafunzi wote, limeendelea kutesa wengi kwani hata matokeo ya mitihani ya upimaji ya kidato cha pili zaidi ya nusu ya watahiniwa walifeli.

Kwa mujibu wa matokeo, watahiniwa 11,245 sawa na asilimia 2.16 wakiwa na daraja A na watahiniwa 9,984 sawa na asilimia 1.92% wakiwa na daraja B.

Aidha watahiniwa 34,783 sawa na asilimia 6.68 wamepata Daraja la C na watahiniwa 48,476  sawa na asilimia 9.32 wamepata Daraja la D.

Hiyo ni sawa na ongezeko la ufaulu la asilimia 0.49% ukilinganisha na asilimia 87.30% ya waliofaulu mwaka jana.

Katika hatua nyingine wanafunzi wengi wamefaulu somo la Kiswahili ikilinganishw ana masomo mengine ambapo Takwimu za somo la Kiswahili zinaonesha kuwa, jumla ya watahiniwa 18,442 (3.54%) wamepata Daraja la A; Watahiniwa 71,745 (13.78%) wamepata Daraja la B, watahiniwa 294,164 (56.52%) wamepata Daraja la C, watahiniwa 113,131 (21.74%) wamepata Daraja la D huku daraja F likiwa na watahiniwa 23,019 sawa na asilimia 4.42.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!