July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Asilimia 80 wamefungwa kwa mauaji Iringa

Mkuu wa Magereza mkoa wa Iringa (PRO), SACP Isidore Mbuhe (katikati) akiwa na waandishi wa habari na maofisa wengine wa jeshi hilo

Spread the love

ULEVI wa kupindukia, wivu wa mapenzi na hasira iliyopitiliza ni miongoni mwa matukio yanasababisha makosa ya mauaji kuongozeka mkoani Iringa. Anaandika Edson Kamukara…(endelea)

Hali hiyo inafanya idadi ya wafungwa waliohukumiwa kwa makosa ya mauji mkoani humo kufikia asilimia 80 ya wafungwa wote hadi sasa.

Takwimu hizi ni kwa mujibu wa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Iringa (RPO), Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP), Isidore Mbuhe, akisema kuwa tabia hiyo ya mauaji kwa kabila la Wahehe imekuwa ya kujirudia.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Iringa, SACP Mbuhe amesema, “hii ni tabia ya Wahehe kujiua kwa kujinyonga au kuua kwa sababu ya kulipiza visasi hasa vya mapenzi. Wanashindwa kuzuia hasira zao”.

“Yaani kwa mfano; mtu anakuomba kitu chako halafu ukimnyima, anajinyonga. Mke au mume akiona mwenzake kasimama mahala anazungumza na mtu, anajinyonga au anamuua mwenzake akidai anamsaliti,” anasema.

Anaongeza uhalifu huo unaongezeka zaidi wakati wa msimu wa pombe ya kienyeji ya ulanzi. Kwamba baadhi ya watu wanashindwa kuzuia hasira zao na hivyo kujikuta wakitenda jinai inayowapelekea kufungwa gerezani.

Kuhusu hali ya msongamano magerezani, SACP Mbuhe amesema kuwa kwa sasa idadi ya wafungwa imepungua, isipokuwa mahabusu ndio wanaongezeka kila wakati.

Anatolea mfano gereza la kilimo Isupilo lililopo wilayani Mafinga, akisema kuwa linahifadhi wafungwa 55 wanaozalisha pamoja na mahabusu zaidi ya 100 hadi 150 wasiofanya kazi yoyote ya uzalishaji.

error: Content is protected !!