Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Asilimia 50 ya watoto wa mitaani wanatokana na ndoa zilizovunjika
Habari Mchanganyiko

Asilimia 50 ya watoto wa mitaani wanatokana na ndoa zilizovunjika

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga
Spread the love

 

MKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga amesema kuwa karibu asilimia 50 ya watoto waishio mitaani zinasababishwa na ndoa zilizovunjika. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Henga ametoa kauli hiyo leo tarehe 25 Oktoba, 2021 jijini Dodoma katika mjadala kuhusu mchango wa asasi za kiraia kwa jamii pamoja na msaada wa kisheria kwa jamii.

Henga amesema asasi za kiraia zimeweza kufanya kazi kubwa ya kuisaidia jamii kwa kutoa msaada wa kisheria pale wanapokuwa wamekwama na wakati mwingine kukosa uwezo wa kumpata wakili.

Amesema kesi nyingi zinatumia muda mwingi kutokana na wanaodai kutokuwa na uelewa wa kisheria na kueleza kuwa kesi ndogo ya kawaida inaweza kuchukua miaka miwili hadi minne.

“Katika kufuatila tumebaini kuwa kesi nyingi ni za migogoro ya mashamba (ardhi), mirathi, ajira na ndoa zilizovunjika.

“Tumebaini karibu asilimia 50 ya watoto wanaoishi mitaani wanatokana na ndoa zilizovunjika kutokana na hilo tumekuwa tukitoa elimu kwenye mabaraza ya ndoa, kutunga sera ya mabaraza ya ndoa kwa kushirikiana na wizara husika ambapo kwa sasa mchakato unaendelea vizuri” ameeleza Henga.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society (FCS), Francis Kiwanga amesema pamoja na Azaki kufanya kazi vizuri na kuwa karibu na taasisi za Serikali lakini Azaki zinatakiwa kuona umuhimu wa maendeleo ya watu na siyo vitu.

Kiwanga amesema Azaki zinatakiwa kuwa kichocheo cha maendeleo ya watu na siyo vitu kwani unaweza kuwa na maendeleo ya vitu wakati watu ni masikini.

“Kwa mfano kuna wakati nilisafiri kutoka Bukoba kwenda Mwanza kwa basi, njiani nilikutana na masoko mazuri cha kushangaza hayakuwa na watu sasa tusijivunie namba za vitu bali maendeleo ya watu” amesema Kiwanga.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa Huru la Kilimo Nchini (ANSAF), Audax Rukonge amesema asasi za kiraia zinatakiwa kujenga tabia ya kuaminiana.

“Pia zinatakiwa kuwa na mawazo ya pamoja na kuwa na uwazi kwa kile wanachokifanya. Ili asasi zifanye vizuri ni lazima zijenge utamaduni wa kuwa na maono ya pamoja, vipaumbele vya pamoja, utekelezaji wa pamoja na kuwa na mifumo ya uwajibikaji wa  pamoja,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Huawei Tanzania yatajwa miongoni mwa waajiri bora kimataifa

Spread the loveKAMPUNI ya Huawei Tanzania imetajwa kuwa mwajiri bora nchini na...

Habari Mchanganyiko

Waziri wa uchumi wa Finland atua nchini, kuteta na mawaziri 7

Spread the loveWAZIRI wa Masuala ya Uchumi wa Finland, Mika Tapani Lintilä...

Habari Mchanganyiko

Asimilia 79 wafeli somo la hesabu matokeo kidato cha nne

Spread the loveWATAHINIWA wa shule 415,844 sawa na asilimia 79.92 ya watahiniwa...

Habari Mchanganyiko

NECTA yafuta matokeo ya watahiniwa 333 kwa kuandika matusi, kudanganya, 286 yazuiwa

Spread the loveBARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta) leo Jumapili limetangaza kuyafuta...

error: Content is protected !!