August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ashikiliwa kwa tuhuma za mauaji Morogoro

Spread the love

HUSSEIN Hassan (38) Mkazi wa Mkwatani, Kilosa mkoani Morogoro anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji, anaandika Christina Haule.

Ulrich Matei, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro amesema kuwa, mauaji hayo yalifanyika tarehe 22 Juni mwaka huu saa 7 mchana katika eneo la Mkwatani Kilosa.

Kamanda Matei amesema, mtuhumiwa akiwa na silaha aina ya shotgun iliyokuwa na risasi 6, alizifyatua ambapo moja ilimpiga Moringe Kandiri (33) mkazi wa Mazoka wilayani humo na kufariki dunia wakati napatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa.

Kamanda huyo amesema, mtuhumiwa huyo anatarajia kufikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika.

error: Content is protected !!