August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ashikiliwa kwa kumpopoa afande

Spread the love

ATHARI Majaribu (17) Mkazi wa Mjimpya Manispaa ya Morogoro anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo huku watu wawili wakitafutwa kwa tuhuma za kumpiga mawe polisi aliyewakamata wakiwa na nyara za serikali, anaandika Christin Haule.

Urlich Matei, Kamanda wa Polisi Morogoro amesema leo kuwa, tukio hilo lilitokea tarehe 19 Mei saa moja asubuhi katika Mji mpya mkoani humo.

Kamanda Mtei amesema kuwa, mtuhumiwa huyo na wenzake wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki moja yenye namba za usajili MC 594 BWD pamoja na kiroba.

Askari mwenye namba F 3453 CPL Ambilikile wa Kituo cha Polisi cha Kati aliyekuwa akiendesha pikipiki yenye namba za usajili MC 405 AZE akitokea Kihonda kwenda kazini, alitilia shaka watu hao na kuanza kuwafuatilia.

Kamanda Mtei amesema, kila alipokuwa akiwaamuru watu hao kusimama, walikataa na kuendelea na safari yao na walipofika maeneo ya Mji mpya alifanikiwa kuwakamata na kuanza kuwahoji ili kubaini nini kilichobebwa na wanakipeleka wapi.

Anasema, wakati akiwahoji ghafla lilitokea kundi kubwa la watu na kuanza kumrushia mawe askari huyo wakimshinikiza kuwaachia watu hao.

Hata hivyo, raia wema waliofika kwenye tukio hilo walipiga simu polisi ambapo walifika eneo la tukio na kumkamata mtu huyo huku wengine wakitoweka na kielelezo.

Polisi waliendesha msako mkali eneo hilo na kufanikiwa kukamata vielelezo ambavyo vilikuwa ni nyama pori ya Kongoni (miguu minne ya mbele na mine ya nyuma) na kwamba, jeshi hilo linaendelea kusaka watuhumiwa wengine.

error: Content is protected !!