Sunday , 3 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Asasi za kiraia kuwasilisha taarifa kila robo mwaka
Habari Mchanganyiko

Asasi za kiraia kuwasilisha taarifa kila robo mwaka

Jiji la Dodoma
Spread the love

WAMILIKI wa Asasi zisizokuwa za kiserikali katika Jiji la Dodoma zimekubaliana kuwa zitakuwa zinawasilisha taarifa zao za kila robo ya mwaka kwa Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hatua hiyo imekuja kutokana na kuwepo muhimu asasi hizo zitambuliwe kazi zao zinazofanyika katika jamii pamoja na uongozi wa Jiji kitengo cha Afisa Maendeleo ya Jamii.

Akizungumza katika kikao hicho Afisa Maendeleo ya Jami Jiji la Dodoma, Sharifa Nabalang’anya alisema kuwa pamoja na serikali kutambua umuhimu wa asasi za kiraia lakini zinatakiwa kutambua kuwa ni muhimu kuwasilisha taarifa zao katika ofisi ya halmashauri ya Jiji.

“Tunajua asasi za kiraia zinafanya kazi kubwa katika jamii, lakini jamii haitambui kazi hizo kwa undani na wakati mwingine hata halmashauri ya Jiji la Dodoma haizijui.

“Ni kwanini kazi za asasi za kiraia hazijulikani kwenye halmashauri ni kutokana na uongozi wa Jiji kutokuwa na taarifa sahihi za utendaji wa kazi zao kutokana na kutowakilisha taarifa zao za utendaji kwa wakati,” alisema Sharifa.

Pamoja na kuwepo kwa utaratibu wa Asasi za kiraia kuwasilisha taarifa zao za utendaji kila baada ya robo mwaka pia asasi hizo zimetakiwa kutumia vyema pesa ambazo zinatolewa na wafadhili badala ya kufanya ujanja ujanja.

Alisema asasi hizo zinatakiwa kuyafikia makundi mbalimbali kama vile vijana wanaojihusisha na dawa ya kulevya, kuvuta bangi na vijana waishio vijiweni kujitambua na kuachana na tabia hizo badala yake wajishughulishe na kazi za kujiingizia kipato.

“Asasi za kiraia mnatakiwa kutambua kuwa nyie ni msaada mkubwa ndani ya serikali na mmekuwa msaada mkubwa kwa maana hiyo naomba mtambue kuwa mnatakiwa kuyafikia makundi maalumu.

“Makundi maalumu siyo watu wenye ulemavu tu bali wapo vijana wanaokaa kijiweni,akina mama na jamii kwa ujumla,kazi kubwa ni kuhakikisha mnatoa msaada chanya kwa jamii ili kuifanya jamii kuwa na maisha mazuri kwa faida ya taifa,” alisema Sharifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

20 wafariki dunia kwa mafuriko Manyara

Spread the loveMVUA za vuli zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimeleta madhara...

ElimuHabari Mchanganyiko

CEO NMB awataka vijana kunoa ujuzi wao

Spread the loveAfisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewashauri...

Habari Mchanganyiko

TARURA kujenga madaraja 189 kwa teknolojia ya mawe

Spread the loveWakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imejipanga kujenga...

AfyaHabari Mchanganyiko

Majaliwa aipongeza GGML mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveWaziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza Kampuni ya Geita Gold Mining...

error: Content is protected !!