January 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Asali ya bilioni 9.8 yauzwa nje

Mizinga ya nyuki

Spread the love

TANI 1,194 za asali zenye thamani ya sh. 9.8 bilioni na tani 644.5 za nta zenye thamani ya sh. 2.6 bilioni, zimesafirishwa nje ya nchi kwa kipindi cha miaka mitatu ya kuanzia 2010 hadi 2013. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika  la Chakula Duniani (FAO), Tanzania ni nchi ya pili kwa ufugaji nyuki barani Afrika baada ya Ethiopia ambapo inazalisha tani 34,000 za asali ambayo ni sawa na asilimia 24.6 ya uwezo wake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Rasilimali za Misitu, Zawadi Mbwambo, amesema, katika juhudi za kuhamasisha ufagaji wa nyuki kwa kipindi hicho, jumla ya manzuki 36 zenye mizinga 4,184 zimeanzishwa nchini katika kanda saba za wakala wa misituTanzania.

Mbwambo ameeleza kuwa kuna jumla ya vikundi 921 nchini vyenye wafugaji nyuki 7,320 kutoka wilaya 30 za mradi wa kuboresha ufugaji wa nyuki vilivyonufaika na ufugaji bora wa nyuki.

Amesema, “jumla ya hekta 69,613 zimehifadhiwa ambapo hekta 37,166 ni za serikali kuu na hekta 23,447 ni hifadhi ya vijiji”.  

Kwa mujibu wa Mbwambo, ufugaji wa nyuki  una mchango mkubwa katika maisha ya binadamu, ambapo huweza kujipatia kipato, chakula  na ajira mwananchi hunufaika na mauzo ya asili anayovuna.

“Sekta ya ufugaji nyuki hapa nchini huajiri watu takribani milioni 4, ukilinganisha na shughuri nyingine za uzalishaji nchini, kwa sababu ufugaji wa nyuki hauitaji mtaji mkubwa wala uangalizi wa kila siku,” amesema Mbwambo.

Ameongeza kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa huduma za misitu Tanzania, itaadhimisha siku ya kutundika mizinga kitaifa Machi 25 mwaka huu, mkoani Tanga.

error: Content is protected !!