May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

AS Vita kutua leo usiku

Kikosi cha AS Vita

Spread the love

 

MSAFARA wa wachezaji 33 pamoja na viongozi wa klabu ya AS Vita kutoka Jamhuri ya Congo, utawasili jijini Dar es Salaama hii leo majira ya saa 1 usiku kwa ajili ya mchezo dhidi ya Simba. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa kundi A, utapigwa siku ya Jumamosi majira ya saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Klabu hiyo inakuja kucheza na Simba huku ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwenye mchezo wa awali kwa bao 1-0, uliopigwa nchini Congo.

Msafara huo wa watu 33, huenda usimuhusishe nahodha na beki wa kulia wa klabu hiyo Djuma Shabani ambaye inasemekana amepata majeraha ya kifundo cha mguu wakati akiwa mazoezini na hivyo anaweza kuukosa mchezo huo dhidi ya Simba.

Kabla ya kuanza safari hiyo kocha wa kikosi hiko, Florent Ibenge alinukuliwa kuwa wanakuja kucheza mchezo huu huku wakiwa wamesahau matokeo ya nyuma waliyoyapata katika mchezo wa kwanza walipokutana.

Kwenye mchezo huo Simba anahitaji pointi moja ili awaeze kufuzu kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Mpaka sasa Simba ipo kileleni ikiwa na pointi 10, baada ya kucheza michezo minne ikifuatiwa na mabingwa watetezi wa kombe hilo, klabu ya Al Ahly wakiwa na pointi saba, huku AS Vita wakiwa kwenye nafasi ya tatu na pointi 4 na Al Merreikh ya Sudan wakishika mkia na kwa pointi moja.

error: Content is protected !!