August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Arsenal yatupwa tena kwa Bayern UEFA

Mechi zilizopita zilizozikutanisha Bayern Munich na Arsenal

Spread the love

HATIMAYE droo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika hatua ya 16 bora imefanyika mchana wa leo, nakushuhudia timu vigogo zitakazomenyana katika hatua hiyo kuelekea fainali ya kombe hilo Juni 3 mwakani kwenye Uwanja wa Millennium ulipo katika mji wa Cardiff nchini Wales.

Michezo hiyo inayotarajiwa kuanza kuchezwa Febuari 14-15 na 21-22 katika mzunguko wa kwanza wa hatua hiyo, huku hatua ya mzunguko wa pili itakuwa Machi 7-8 na 14-15, na baada ya hapo itaingia hatua ya robo fainali.

Licha ya kuongoza kundi lao klabu ya Arsenal imejikuta imeangukia tena katika mikono ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani, huku Paris Saint Germain (PSG) itavaana na FC Barcelona, mabingwa watetezi Real Madrid wao watakipiga na Napol ya Italia, Leicester City wataikabili Sevilla, Bayern Leverkusen dhidi ya Atletico Madrid, FC Porto na Juventus, Manchester City watamenyana na Monaco na Benfica watawakalibisha Borrusia Dortmund.

Michezo inayoonekana kuvutia wapenzi wengi wa mpira ni Arsenal dhidi ya Bayern Munich kutokana na historia zao, katika michezo 11 waliokutana katika michuano hii toka mwaka 2000, Arsenal wamefanikiwa kushinda mechi tatu, huku Bayern Munchen ikishinda michezo mitano na kwenda sare mara mbili.

Lakini pia mchezo mwingine utakao kuwa kivutio kwa wengi na wenye ushindani mkubwa ni ule utakao wakutanisha matajiri wa ufaransa PSG dhidi ya FC Barcelona, licha ya PSG kutokuwa na rekodi nzuri katika michuano hiyo wanapokutana na Barcelona kwa misimu kadhaa.

Katika michezo nane waliokutana katika historia ya michuano hiyo katika hatua tofauti, Barcelona amefanikiwa kushinda michezo mitatu huku PSG akishinda michezo miwili na kwenda sare mechi tatu, kama PSG watafanikiwa kumfunga Barcelona basi watakuwa wamefuta uteja mbele ya mabingwa hao wa Hispania.

error: Content is protected !!