Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo Argentina bingwa wa dunia, Messi aweka historia
MichezoTangulizi

Argentina bingwa wa dunia, Messi aweka historia

Spread the love

 

TIMU ya Taifa ya Argetina imevunja rekodi ya miaka 36 iliyopita baada ya kuinyuka Ufaransa jumla ya penalti 4 – 3 na kubeba kombe la Dunia kwa mara ya tatu.

Hatua hiyo imekuja baada ya timu hizo kufungana bao 3-3 katika muda wa dakika 120. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Fainali hiyo iliyopigwa leo tarehe 18 Disemba, 2022 katika Uwanja wa Lusail nchini Qatar kuanzia saa 12:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, imekuwa ya kipekee kwa ubora wa soka uliooneshwa na timu zote huku mvua ya magoli ikimiminika.

Hata hivyo, ‘battle’ kubwa ilikuwa kati ya staa wa dunia Leonel Messi na Kylian Mbappe ambao wote kabla ya mchezo huo walikuwa wanaongoza kwa ufungaji katika fainali hizo kwa kuwa na mabao 5 kila mmoja.

Hata hivyo, ni Mbape ndiye aliyeibuka kinara kutupia nyavuni bao 3 na kufikisha mabao 8 huku Messi akifunga mabao 2 na kufikisha mabao 7.

Argentina walikuwa wa kwanza kupata bao ambapo dakika 23 Messi alitupia bao kwa njia ya penalti baada ya Ousmane Dembélé kumkwatua Angel Di Maria ndani ya eneo la 18.

Lionel Messi

Dakika ya 36 Di Maria ambaye alikuwa mwiba mkali kwa Ufaransa katika kipindi cha kwanza alitupia bao la pili na kuifanya timu yake kwenda mapumziko kwa uongozi mnono.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ya ajabu ambapo Ufaransa walifanya mabadiliko yaliyorejesha uhai hasa ikizingatiwa kipindi cha kwanza kilitamatika bila kupiga mpira wowote langoni mwa Argentina.

Dakika ya 80 Mbape aliwainua mashabiki wa Ufaransa baada ya kupata penalt lakini sekunde 97 baadaye akatupia la pili na kuufanya uwanja kuwa “level”.

Baada ya kwenda dakika 30 za nyongeza Messi alipata bao dakika ya 108 lakini Mbape naye akajibu mapigo dakika ya 118 baada ya mchezaji wa Argentina kupangua shuti la Mbape kwa kiwiko kisha Ufaransa kupewa penalti.

Timu hizo zilipoingia kwenye matuta, vinara hao Mbape ma Messi walikuwa wa kwanza lupiga penalti ambapo wote walipata.

Kilio kilianza kwa Ufaransa baada ya Emiliano Martinez kupangua penali ya Kingsley Coman huku Aurelien Tchouameni akikosa baada ya kupiga nje.

Hii ni mara ha tatu kwa Argentina kutwaa kombe la dunia, mara ya kwanza ilibeba mwaka 1978, ya pili 1986 na ya tatu 2022.

Aidha, ni mara ya kwanza kwa Messi kubeba kombe hilo tangu aanze kucheza mpira.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!