July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ardhi yatawala Tamasha la Nyerere

Mwananchi wa Loliondo, Kooya Timan

Mwananchi wa Loliondo, Kooya Timan (mwenye kipasa sauti) akitoa malalamiko yake kuhusu wananchi wa Loliondo kunyang'anywa ardhi yao

Spread the love

UBINAFSISHAJI katika sekta ya ardhi umeshidwa. Ardhi imetakiwa kumilikiwa na umma badala ya Serikali. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaa na washiriki wa Tamasha la saba la Mwalimu Julius Nyerere, linaloandaliwa na Kigoda cha Mwalimu Nyerere.

Mada kuu ya mwaka huu ni “Ubinafsishaji wa Haki za Kijamii kwa Wanyonge” ambayo inalenga kuangalia namna ubinafsishaji katika masuala ya ardhi na madini unavyowaathiri wananchi wa tabaka la chini.

Akieleza kuhusu kushidwa kwa ubinafsishaji, Kooya Timan – mwananchi kutoka kijiji cha Ololosokwan, Loliondo mkoani Arusha, anasema,  “wakazi wa Loliondo tumeathirika sana na ubinafsishaji na suala zima la uwekezaji”.

“Tumeondolewa kwenye maeneo yetu ya asili. Maeneo haya wakapewa wawekezaji wa makampuni ya OBC kutoka Uarabuni na Thomson kutoka Ujerumani. Baada ya kukataa kuondoka, tunaambiwa sisi ni wakenya. Sio Watanzania. Hatuoni faida ya ubinafsishaji wala uwekezaji. Tunadai haki ya kumiliki ardhi,” amesema Timan.

Aidha, Timan amesema “tunaishangaa serikali kutetea wawekezaji wawili badala ya maelfu ya wananchi wake.Tunasomesha watoto. Hatuna uchumi mwingine. Tunawaomba wasomi mtusaidie katika mapambano haya”.

Aidha, Peter Kayiira kutoka kijiji cha Mubende, Uganda amesema “Tumekuwa katika mapambano ya kutetea ardhi yetu kwa miaka 14. Hii ni baada ya serikali kuvunja katiba na kupora ardhi yetu kwa kutumia jeshi na kumpa mwekezaji wa kilimo cha chai”.

“Katiba na Sheria za Uganda zinatambua ardhi ni mali ya umma. Lakini serikali ilizivunja. Uporaji huu ulifanyika mwaka 2001. Zaidi ya familia 4000 ziliathirika. Wakati nikitetea ardhi yetu nikakamatwa na kuwekwa kizuizini lakini nikashinda kesi. Kwa hali hii sisi kama wananchi hatunufaiki na ubinafsishaji na uwekezaji,”anasema Kayiira.

Joseph Butiku – Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere amesema “Nyerere hakuchukia uwekezaji. Alizungumzia na kuamini uwekezaji wenye maslahi kwa wote. Kama tungeweka kufuata mtizamo wa Nyerere kuhusu uwekezaji, basi tungetatua migogoro hii”.

Aidha, Samuel Kasori – aliyekuwa Katibu wa Mwl Nyerere amesema “ Nyerere hakujilimbikizia ardhi. Mpaka umauti unamfika alimiliki nyumba moja tu ya Msasani Jijini Dar es Salaam”.

“Alikodi mashamba yenye ekari 128 kutoka serikali ya kijiji cha Butiama kwa ajili ya kulima. Kabla ya kifo chake aliyarejesha. Hata ile nyumba ya Butiama alirithi kwa baba yake. Lakini viongozi wa sasa hawaishi kama Mwalimu. Wanaongoza kwa ufisadi wa kupora na kujilimbikizia ardhi,” amesisitiza Kasori.

error: Content is protected !!