October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Aprili Mosi siku ngumu kwa Halima Mdee

Halima Mdee, Mbunge wa Kawe akiwa mahakamani Kisutu

Spread the love

APRILI Mosi mwaka huu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam itaamua kama Halima Mdee, Mbunge wa Kawe ana kesi ya kujibu ama la! Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Mdee anadaiwa tarehe 3 Julai 2017, katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alitoa alitoa lugha ya matusi dhidi ya  Rais John Magufuli.

Alitamka kwamba ‘anaongea hovyo, anatakiwa afungwe breki,’ kitendo kinachodaiwa kuwa ni udhalilishaji kwa Rais Magufuli na kwamba, kauli hiyo ingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Leo tarehe 20 Februari 2020, mbele ya Hakim Mkazi Mkuu Thomas Simba, wakili wa serikali mwandamizi Wankyo Simon amedai, upande wa mashitaka umefunga ushahidi wa mashahidi watatu katika kesi hiyo.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili Mosi 2020, kwa ajili ya kutoa uamuzi kama Mdee ana kesi ya kujibu ama la.

error: Content is protected !!