March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Anthony Joshua aendeleza rekodi ya kibabe

Spread the love

BONDIA wa Uingereza, Anthony Joshua (28), usiku wa kuamkia Jumapili Septemba 23, 2018, ameendeleza ubabe kwa kumtwanga Alexander Povetkin (39) kwa KO (Knock Out) katika raundi ya saba. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mpambano huo wa uzito wa juu wa raundi 12 uliochezwa nchini Uingereza, uliwakutanisha wababe hao wenye rekodi nzuri za ushindi ambapo kabla ya mchezo huo, Joshua alikuwa na rekodi ya kucheza michezo 21 bila kupoteza wakati Povetkin akicheza michezo 37 na kupoteza mmoja.

Mpambano huo uliohudhuriwa na watazamaji 80,000 ulimshuhudia Povetkin maarufu kama Simba Mweupe, akianza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kumchana pua ya Joshua katika raundi ya pili baada ya kumshushia konde zito.

Joshua mwenye asili ya Nigeria alicharuka na kufanikiwa kumuangusha mara mbili mpinzani wake kabla ya mwamuzi kukatisha pambano kwenye mzunguko wa saba ili kunusuru uhai wa Povetkin.

Kwa ushindi huo, Joshua amefanikiwa kujiingizia kitita cha Pauni za Uingereza 20 milioni (sawa na Sh. 59.6 bilioni) huku mpinzani wake akiingiza pauni 6 milioni (sawa na Sh. 17.8 bilioni).

Joshua ambaye Mama yake ni Mwafrika kutoka nchini Nigeria ameendelea kushikilia mikanda yake mitatu ya Uzito wa juu inayotambulika na WBC, WBA na IBF.

error: Content is protected !!