January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Angola, Rwanda, DRC, Rwanda, Kenya zanufaika chanzo ya corona

Spread the love

 

NCHI kadhaa Afrika ikiwa ni pamoja na Rwanda, Kenya, Uganda, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), tayari zimepokea chanjo ya virusi vya corona (COVID-19). Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Chanjo hiyo aina ya AstraZeneca tayari imesambazwa kwenye mataifa hayo, ambapo Kenya imepokea jumla ya dozi milioni 1.02.

Katika mgao wa chanjo hiyo, DRC imepokea dozi milioni 1.7 kati ya dozi mil 6.9 za chanjo hiyo usiku wa jumanne tarehe 2 Machi 2021. chanzo hiyo imepokewa na Waziri wa afya wa nchi hiyo, Eteni Longondo.

Angola imepokea jumla ya dozi 624,000 huku Gambia ikiwa imepokea dozi 36,000 leo Jumatano tarehe 3 Machi 2021.

Pia leo Jumatano asubuhi, Rwanda imepokea dozi yake ya kwanza ya chanjo ya Oxford-AstraZeneca huku ikitarajia dozi 102,960 za chanjo ya Pfizer, kulingana na Wizara ya Afya ya nchi hiyo.

Rwanda inatarajia kupokea jumla ya chanjo 1,098,960 za AstraZeneca na Pfizer, katika mpango wa Covax unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa (UN). katika mpango wa chanjo hiyo, Tanzania haimo.

error: Content is protected !!