Saturday , 10 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Anglikana wamchoka Askofu Mokiwa
Habari Mchanganyiko

Anglikana wamchoka Askofu Mokiwa

DK. Valentino Mokiwa, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam (katikati) akiendesha misa
Spread the love

DK. Valentino Mokiwa, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam amechokwa na kanisa lake, anaandika Faki Sosi.

Tayari waraka wa kumng’oa kwenye mamlaka hayo umetolewa huku akibebeshwa tuhuma 10, miongoni mwazo ni ubadhirifu wa mali za kanisa na matumizi mabaya ya madaraka.

Taarifa kutoka ndani ya kanisa hilo zinaeleza kuwa, uamuzi wa Mokiwa kuvuliwa madaraka ya kanisa hilo umefanywa na maaskofu wakuu wa kanisa hilo mwanzoni mwa mwezi huu.

Pamoja na baadhi ya watumishi ndani ya kanisa hilo akiwemo Yohana Sanga ambaye ni Ofisa Habari wa Mokiwa kupinga kuwepo kwa taarifa hiyo, taarifa zaidi zinaeleza kuwa tayari Mokiwa amevuliwa uongozi.

“Waraka umeishaandikwa na umefikishwa sehemu husika, ameupata na utekelezaji wake umeanza,” kinaeleza chanzo chetu ndani ya kanisa hilo.

Sababu zingine zilizoelezwa kwenye waraka huo ni pamoja na kuandamwa na tuhuma za migogoro na kutokuwa na maelewano ndani ya dayosisi aliyokuwa akiiongoza, kuzuia dayosisi kupeleka michango jimboni bila maelezo ya Sinodi ya Dar es Salaam.

Mokiwa anadaiwa kuingia mikataba kiholela kinyume na kifungu cha 29 na 32 cha kanisa hilo pia kufuja mali za kanisa.

Tuhuma zingine za Mokiwa ni kushawishi dayosisi hiyo kujitoa kwenye udhamini wa Kanisa Anglikana Tanzania kinyume na katiba ya dayosisi hiyo pia anatajwa kushindwa kutatua migogoro ya mapadri na waumini.

Sehemu ya waraka huo imeeleza kuwa “pia aliwahi kushtakiwa na Mchungaji Christopher Mtikila, Erasto Mhagama, Christopher Njavike na George Mwafalo kwa kosa la kuwatishia silaha ya moto na kuwapapasa maungoni bila ridhaa yao kinyume na maadili ya kanisa.”

Kwa sasa Dayosisi ya Dar es Salaam ipo chini ya uongozi wa askofu mkuu mpaka pale hatua mahususi za kumpata kiongozi mwingine zitakapokamilika.

Waraka uliomwondoa Mokiwa madarakani ulipewa kichwa cha habari ‘Taarifa fupi ya Askofu Mkuu kuhusu kuamuru Askofu Dk. Valentino Mokiwa Dayosisi ya Dar es Salaam kujiuzulu’ umeasiniwa na Mchungaji John Chinyang’ole ambaye ni Katibu Mkuu wa Kanisa hilo.

Pia waraka huo umefikishwa kwa Baba Askofu wa Kanisa Anglikana Tanzania, Msajili wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Katibu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi zaidi ya 100 wapigwa msasa wa udereva kukabiliana na ajali

Spread the love  KATIKA kuhakikisha wimbi la ajali za barabarani zinapungua kama...

Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali yakana kuhamisha kwa nguvu jamii ya Kimasai Loliondo

Spread the loveWAZIRI wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro,...

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

error: Content is protected !!