KANSELA wa Ujerumani, Angela Merkel amempongeza mgombea wa ukansela aliyekuwa mpinzani wake kupitia chama cha Social Democratic SPD Olaf Scholz. Anaripoti Helena Mkonyi, TUDARCo … (endelea)
Ni baada ya kushinda uchaguzi uliofanyika Jumapili ya tarehe 26 Septemba, 2021.
Jana Jumatatu, tarehe 29 Septemba 2021, ofisi ya Merkel imeeleza Kansela Angela Markel anayeondoka madarakani, aliwasiliana binafsi na Scholz ambaye ni waziri wake wa fedha kwa sasa aliyeshinda ukansela wa Marekani, katika uchaguzi huo.
Ofisi hiyo ilisema, Merkel na mawaziri wataendelea na majukumu yao hadi serikali mpya ya shirikisho itakapoundwa na kuchukua rasmi madaraka.
“Kansela Merkel ataendelea kutekeleza majukumu yake ikiwemo kufanya ziara za nje na kuhudhuria mikutano ya viongozi wa serikali wa nchi nyingine.”
Aidha, kiongozi wa Christian Democratic Union (CDU), Armin Laschet pia amempongeza Olaf Scholz kwa kushinda nafasi ya ukansela.
Leave a comment