CHAMA cha African National Congress (ANC) ambacho kinatawala nchini Afrika Kusini cha kimepoteza udhibiti baada ya kushidwa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Pretoria, anaandika Pendo Omary.
ANC kimeshindwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa katika eneo hilo, baada ya kuzidiwa nguvu na chama cha Democratic Alliance ambapo matokeo yanaonesha kuwa chama cha Democratic Alliance kikipata 43 asilimia ya kura na ANC 41 asilimia.
Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limeripoti kwamba chama cha Democratic Alliance kitalazimika kuunda serikali ya mseto kuongeza udhibiti katika eneo hilo, ambapo pia ANC na Democratic Alliance vinachuana vikali kudhibiti mji wa Johannesburg, ambao ni mji mkubwa kabisa nchini humo.
Katika uchaguzi huo ANC kikiwa moja kati ya vyama vikogwe vilivyo madarakani barani afrika kimepata matokeo mabaya zaidi tangu kuanzishwa kwake.
More Stories
Uholanzi, Uturuki ‘waingia’ vitani
Mauaji ya Jamal Khashoggi, CIA yaivua nguo Saudia Arabia
Marekani yafanya ‘uchochezi,’ yawaonya wanaokuja Tanzania