Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Amuua mkewe, ajinyonga
Habari Mchanganyiko

Amuua mkewe, ajinyonga

Emmanuel Nley, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora
Spread the love

SAID Ramadhan, Mkazi wa Kijiji cha Ikongoro wilayani Uyui amejinyonga baada ya kumuua mkewe Mwajuma Hussein kwa kumpiga risasi kutokana na wivu wa mapenzi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa ya tukio hilo imetolewa jana tarehe 24 Agosti, 2014 na Emmanuel Nley, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora wakati akizungumza na wanahabari.

Akizungumzia kuhusu tukio hilo, Kamanda Nley matukio hayo yalitokea Agosti 21 mwaka huu ambapo mwili wa marehemu Mwajuma Hussein uliokotwa kwenye msitu wa Isawima katika kitongoji cha Kombe kata ya Igagala mkoani Tabora.

Kamanda Nley alieleza kuwa, baada ya marehemu Ramadhan kumuua mkewe, alikimbilia porini akiwa na bunduki aina ya gobore aliyokutwa nayo ikiwa pembeni ya mti alioutumia kujinyonga.

Alisema kuwa, uchunguzi wa awali umeonyesha chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi kwani kabla Ramadahi ambaye sasa ni marehemu hajamuoa Mwajuma naye Marehemu alikuwa ameolewa na Jumanne Malawiro ambaye walizaa naye watoto wawili.

Alisema kuwa marehemu Ramadhan alihisi kuwa uenda mkewe bado ana mahusiano ya kimapenzi na mzazi mwenzie huyo ndipo akaamua kumuua na kisha yeye kujiua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!