March 2, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Amunike kuwapa nafasi nyingine nyota wa Simba

Clifford Ndimbo, Msemaji wa TFF (kulia) akiwa na Msemaji wa Simba, Haji Manara

Spread the love

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars, Emmanuel Amunike  ametoa msamaha kwa wachezaji wa watano wa Simba na mmoja wa Yanga aliowaondoka katika kikosi chake baada ya kuchelewa kuripoti kambini. Anaripoti Halidi Mhina …. (endelea).

Wachezaji walioondolewa katika kikosi cha Amunike ni Faisal Salum wa Yanga, Shiza Kichuya, Johhn Bocco, Hassan Dilunga, Shomari Kapombe, Jonas Mkude pamoja na Erasto Nyoni wote hao kutoka Simba.

Msemaji wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo, amesema tatizo kazi ya wachezaji hao na Kocha Amunike limemalizika baada ya kocha huyo kukutana na nyota hao na ameahidi atawapa nafasi nyingine ya kujiunga na kikosi chake kama wataonesha tena kiwango kizuri kwenye klabu zao.

Lakini pamoja na msamaha huo nyota hao hawatajumuishwa kwenye kikosi kitakacho kwenda kuwavaa timu ya Taifa ya Uganda kwenye mchezo wa kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa Afrika ‘AFCON’ unaotarajiwa kuchezwa Septemba 8, 2018 kwenye uwanja wa Nelson Mandela uliopo Nambole.

Naye Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema kuwa Simba hawana tofauti yoyote na kocha wala uongozi wa TFF kwa kilichotokea na kudai kuwa wameweka silaha chini na wote wanashirikiana kuiunga mkono timu ya Taifa.

error: Content is protected !!