Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Michezo Amunike amtosa Kichuya, awarudisha nyota wa Simba
Michezo

Amunike amtosa Kichuya, awarudisha nyota wa Simba

Spread the love

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Emmanuel Amunike ametangaza majina ya wachezaji 30 watakaoingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Cape Verde, huku jina la kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba Shiza Kichuya likikosekana kwenye orodha hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Kukosekana jina la mchezaji huyo katika kikosi kilichotangazwa na Amunike pengine kinaweza kutafsiriwa kuwa kiwango chake kimeshuka kwa siku za hivi karibuni katika klabu yake ya Simba hivyo kutopata nafasi ndani ya Stars.

Mchezo huo wa Tanzania na Cape Verde unatarajiwa kuchezwa 12 Oktoba, 2018 na siku nne baadae watarudiana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho ni sambamba na walinda mlango, Aishi Manula, Beno Kakolanya, Mohamed Abdulahman, huku walinzi wakiwa ni Hassan Kessy (Nkana), Shomari Kapombe (Simba), Salum Kimenya (Prisons), Gadiel Michael (Yanga), Paulo Ngalema, Ally Sonso (Lipuli), Aggrey Morris, David Mwantika, Abdallah Kheri (Azam), Kelin Yondani, Andre Vicent (Yanga) na Abdi Banda (Baroka).

Viungo wapo Himid Mao (Petrojet), Saimon Msuva (El Jadida), Mudathir Yahya, Frank Domayo (Azam), Jonas Mkude (Simba), Feisal Salum (Yanga), Salum Kihimbwa (Mtibwa Sugar) na Farid Musa (Tenerife).

Huku washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk), Thomas Ulimwemgu (Al Hilal), John Bocco (Simba), Yahya Zayd (Azam), Kelvin Sabato (Mtibwa Sugar), Rashid Mandawa (BDF XI) na Shaban Chilunda (Tenerife).

Stars ambao mpaka sasa wana alama mbili baada ya kwenda sare katika michezo miwili ya awali inahitaji kushinda mchezo huo ili iweze kujitengenezea nafasi nzuri ya kufuzu kwa mara ya pili katika michuano hiyo ya kombe la mataifa Afrika AFCON.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Anza Jumamosi yako na mkwanja wa Meridianbet

Spread the loveJumamosi ya leo ODDS zimekaa kijanja sana ndani ya Meridianbet...

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

error: Content is protected !!