July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Amri ya mita 200 yalalamikiwa

Spread the love

WANANCHI walalamikia kauli ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ya kuwataka wananchi kuondoka umbali wa mita 200 sawa na viwanja viwili vya mpira kuwa ni kukandamiza demokrasia. Anaandika Faki Sosi … (endelea)

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na MwanaHALISI Online wanesema kujua na kulinda kura zao haki yao kutokana na serikali iliyo madarakani kutofuata misingi ya haki kwa kubana uhuru wa wapigakura.

Anwar Mchakama, mkazi wa Tandika amesema suala kuwa wananchi hawana imani na tume kutokana na kuizika misingi ya demokrasia ya uchaguzi huru na wa haki.

“Sisi wapigakura hatupo tayari kuwaona mawakala wanaosimamia kura zetu wanatishwa katika mazingira ya kutaka kumfanya aachie mawakala na wasimamizi wa CCM waibe kura zetu,’’ amesema Mchakama.

Aramu Aroni ambaye ni mfanyabiashara maeneo ya Temeke amesema tayari Jeshi la Polisi limeshaanza kutisha wananchi kutokana na tukio lilitokea usiku wa kuamkia jana walipowakamata na kuwadhalilisha wafanyabiashara katika maeneo ya Chihota nyakati za usiku wakidai kuwa ni wazururaji ilhali waliwakuta katika shughuli zao za biashara.

“Tayari wananchi tunapata vitisho kutoka serikali hii ya CCM kutokana na kipindi hiki kuelekea uchaguzi kuna kamatakamata isiyokuwa na sababu, mtu anayefanyabiashara huwezi kusema ni mzururaji,” amesema Aroni.

Mkazi wa Mwanyamala, Justine Nyirabu ameonesha wasiwasi wa hali hiyo akisema ni mpango wa CCM kupitisha masanduku yenye kura feki ili wananchi wasijue.

Denis Chilole wa Karagwe amesema suala la kuzuia wananchi kukaa nje ya mita 200 linaweza kuleta mgogoro mkubwa kutokana na vituo vingi vya kupigia kura kuwepo karibu na makazi ya watu hata chini ya masafa hayo.

Naye Kondo Bungo ni mgombea ubunge jimbo la Mbagala kupitia UKAWA kwa tiketi ya CUF, ambaye anasema wananchi jimboni kwake hawajakubliana na amri ya kukaa mbali na kituo kwa kuwa umbali huo hauwawezeshi kufuatilia matokeo ya kura zao.

Amesema wala wananchi hawataweza kusoma matokeo yaliyobandikwa kwenye kuta za kituo cha kupigakura pia kutomsikia msimamizi wa kituo cha kupigakura akitangaza matokeo ambayo ni haki yao ya kikatiba kusikiliza.

error: Content is protected !!