Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Amnesty: Kunyamazisha wakosoaji ni tusi
Habari za Siasa

Amnesty: Kunyamazisha wakosoaji ni tusi

Spread the love

KUENDELEA kuwekwa kuzuizini kwa mwanasheria wa haki za binadamu, Tito Elia Magoti na mwenzake Theodory Giyani, ni jaribio la kutaka kunyamazisha wakosoaji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ni kauli ya shirika la lisilo la kiserikali la masuala ya haki za binadamu la kimataifa – Amnesty International, tarehe 21 Januari 2020, wakati watuhumiwa walipofikishwa mahakamani.

Tito na Giyani, ambao ni wayefanyakazi kwenye Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), walifikishwa katika Mahakama ya Kisutu kwa tuhuma za kuongoza genge la uhalifu, kumiliki programu ya kompyuta iliyobuniwa kwa lengo la kutenda uhalifu na utakatishaji fedha.

“Ni tusi kwa haki na ni jaribio la wazi la kuwanyamazisha wakosoaji wa serikali kwa kuwaweka kizuizini,” taarifa ya shirika hilo imeeleza, kwa mara ya kwanza walishikiliwa tarehe 20 Desemba 2019.

Amnesty imeeleza kuchukizwa na matumizi ya sheria ya kushughulikia uhalifu, kwa kuwaweka ndani wakosoaji kwa muda mrefu kwa makosa yasiyo na dhamana, kwa madai ya kutokamilika upelelezi.

“Kufanya hivi ni kukiuka kabisa utaratibu unaozingatia sheria na upotoshaji wa haki,” amesema Seif Magango, Naibu Mkurugenzi wa Amnesty International katika Kanda ya Afrika Mashariki kwenye taarifa hiyo na kuongeza kuwa mamlaka husika zinapaswa kuwaacha Magoti na Giyani bila masharti.

Tito na Giyani walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza tarehe 24 Desemba 2019, na kusomewa mashtaka matatu ambapo tarehe 7 Januari 2020, mahakama ya jijini Dar es Salaam iliahirisha kesi yao baada ya upande wa mashtaka kuomba muda zaidi wa kukamilisha upelelezi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!