December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Amfyeka mumewe korodani kisa hamridhishi kitandani

Spread the love

 

MWANAMKE mmoja raia wa Kenya aliyefahamika kwa jina la Karambu Meme (40) anadaiwa kumshambulia na kumkata korodani mumewe Meme Kabati (56) kwa madai kuwa hajawahi kumridhisha wanapokuwa katika tendo la ndoa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Mwanaume huyo amelazwa katika hospitali ya Nyambene kaunti ya Meru nchini humo baada mkewe huyo kumvuta na kuikata korodani yake moja.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Chifu Msaidizi wa eneo la Ntunene kulipotokea tukio hilo, Edward Mutalii alisema baada ya kupokea taarifa hizo za kutatanisha, alienda haraka eneo la tukio na kukuta sehemu ya korodani ya muathiriwa ikiwa chini.

Polisi wamemkamata mwanamke huyo na kwa sasa anashikiliwa akisubiri kufikishwa mahakama lakini mwanamke huyo amesisitiza kuwa amefanya hivyo kwa kuwa kamwe mumewe hajawahi kumridhisha wakati wakiwa katika ktendo la ndoa.

error: Content is protected !!