
Shamba la mahindi
TAASISI ya kuendeleza mifumo ya masoko kwenye kilimo nchini (AMDT), imepanga kuwafikia wakulima 500,000 wa zao la alizeti wa mikoa 12 ya Tanzania bara katika kipindi cha miaka mitano 2016- 2021, anaandika Mwandishi Wetu
Hayo yamebainishwa na Meneja Programu wa taasisi hiyo, Martin Mgallah, wakati alipokuwa akiwasilisha taarifa yake wakati wa uzinduzi wa progamu ya alizeti AMDT.
Mgallah amesema taasisi hiyo imelenga kufanya kazi katika mikoa yote ya Tanzania bara na kwa awamu ya kwanza ya miaka mitano itaanza na mikoa 12.
Ametaja mikoa hiyo kuwa ni Songwe, Mbeya, Rukwa, Katavi, Njombe, Iringa, Dodoma, Singida, Shinyanga, Manyara, Lindi pamoja na Mtwara.
“Tunategemea kufikia wakulima 500,000 wa zao la alizeti ambao watanufaika na taasisi hii kwa kupata mafunzo ya kilimo bora pamoja na matumizi ya mbegu bora kwa kuzingatia kanuni bora ili kuwa na matokeo chanya”alisema Mgallah.
Aidha, amesema kuwa taasisi hiyo inafadhiliwa na serikali za nchi nne ambazo ni Denmarrk, Sweden, Uswisi na Ireland ikishirikiana na serikali ya Tanzania kupitia Wizara na taasisi zake.
More Stories
Dk. Mpango azitaka mamlaka maliasili utalii kukomesha urasimu vibali
TANESCO yaghairi matengenezo mfumo wa LUKU
Morogoro yapokea bilioni 111 miradi ya maendeleo