January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kamati yaibana Serikali ipunguze matumizi

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya akiingia bungeni kusoma bajeti

Spread the love

KAMATI ya Kudumu ya Bajeti, imeitaka Serikali kupunguza matumizi na kuacha kufanya matumizi siyoidhinishwa ili fedha zinazotegwa zielekezwe kwenye matumizi ya maendeleo. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Kidawa Hamid Salehe, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, ndiye amesasilisha maoni na mapendekezo ya kamati zikiwa siku tano tangu Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya awasilishe Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2015/16 ya Sh. 22.4 trilioni.

Amesema taarifa ya mwenendo wa uchumi kwa mwaka wa fedha 2014, inaonesha pato la taifa likikuwa kwa asilimia 7, kiwango ambacho ni kidogo kikilinganishwa na takwimu za mwaka 2013, ambapo pato hilo lilikuwa kwa asilimia 7.3 huku mfumuko wa bei ukiwa asilimia 6.1, ikilinganishwa na asilimia 7.9 kwa mwaka 2013. 

“Agosti mwaka huu, mfumko wa bei ulikuwa asilimia 4.8. Hii inatokana na kupanda na kushuka kwa mafuta katika soko la dunia na kupanda kwa gharama za chakula,” ameeleza Kidawa. 

Aidha, amesema kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya kimarekani kwa kiasi kikubwa kumeathiri uchumi katika kuagiza bidhaa, kuongeza malipo ya mikopo ya nje na kuathiri uwekezaji.

Akieleza kuhusu maoni ya kamati hiyo, Kidawa amesema Sheria ya Elimu na Ufundi inapaswa kutoa msamaha wa kodi kwa elimu ya ufundi ili kutoa unafuu kwenye kilimo, kwamba serikali ifufue na kuanzisha viwanda vya ngozi, ifuatilie ajira zinazotolewa na wawekezaji na fedha zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo.

Mapendekezo mengine ni: serikali kupeleka umeme vijijini, iandae mfuko wa uwekezaji, kuanzishwa kwa benki ya kilimo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kusimamia ipasavyo makusanyo ya mapato ya kodi na serikali kuongeza ushirikishwaji.

Wakati huohuo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, nayo imewasilisha maoni yake kuhusu Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2015/2016.

Akiwasilisha maoni hayo, Esther Matiko, Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni katika Ofsi ya Rais – Mahusiano na Uratibu, amesema kambi inaitaka serikali kugharamia mpango huo kwa fedha za ndani angalau kwa asilimia 50. 

“Serikali igharamie mpango huu angalau kwa asilimia 50 kuliko ilivyo sasa ambapo inagharamia asilimia 32.5 tu. Athari za kuacha asilimia kubwa ya ugharamiaji wa Mpango itolewe na wahisani, miradi ya maendeleo haitekelezwi hasa ukizingatia kwamba wengi wa wafadhili wamesitisha misaada ya maendeleo kutokana na kukithiri kwa rushwa na ufisadi serikalini,” amesema Matiko. 

Ameongeza kuwa, Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2011/12 – 2015/16 ulikadiriwa kugharimu Sh. trilioni 8.9 kila mwaka ambapo Sh. trilioni 2.9 zilitakiwa kutokana na fedha za ndani katika bajeti ya serikali na Sh. trilioni 6 zilitakiwa kutokana na uwekezaji wa sekta binafsi na washirika wa maendeleo. 

“Kwa takwimu hizo tu, inaonyesha kwamba taifa linagharamia Mpango wake wa Maendeleo kwa asilimia 32.5 tu.  Asilimia 67.5 ya gharama za utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa zinategemewa kutokana na misaada na mikopo kutoka kwa washirika wa maendeleo ambayo haina uhakika wa kutolewa kwa asilimia 100,” ameeleza Matiko.

Pia, ameeleza kuwa licha ya tengeo dogo la fedha za ndani kugharamia mpango, bado fedha hizo hazitolewi kwa wakati jambo ambalo linakwamisha miradi mingi ya maendeleo.

Anasema “kwa mfano mapitio ya ugharamiaji wa Mpango mwaka 2014/15 yanaonyesha kwamba ni asilimia 39 tu ya bajeti ya maendeleo iliyokuwa imetolewa na Serikali hadi kufikia Machi, 2015. Hata hivyo, hakuna uhakika kama asilimia 61 ya bajeti ya maendeleo iliyobaki inaweza kutolewa kabla ya mwaka huu wa fedha kumalizika.” 

Matiko amesema, kimsingi serikali imeshindwa kabisa kutekeleza ibara ya 19 ya iIani ya CCM. Kwa mfano, kuongeza uwezo wa maarifa (sayansi na teknolojia) katika nchi kwa kutilia mkazo ubora wa Elimu na Raslimali Watu ya nchi kama ilani yao inavyosema.

Hii ni kwa sababu miaka kumi ya utawala wa serikali hii ya awamu ya nne ya CCM ndiyo kipindi ambacho elimu ya Tanzania imeporomoka kuliko miaka yote katika historia ya nchi. Ndiko tumeshuhudia asilimia 65 ya wanafunzi wa kidato cha nne wakipata daraja sifuri mwaka 2012,”amefafanua Matiko.

error: Content is protected !!