August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Amana One Stop Center wapigania wabakwaji

Spread the love

JAMII imetakiwa kutoa taarifa za watoto wanaobakwa na au kulawitiwa mapema ili kuwezesha upatikanaji wa ushahidi, anaandika Regina Mkonde.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Sophian Mndolwa, Ofisa Ustawi wa Jamii wa Kituo cha Amana One Stop Center amesema kuwa, kumekuwepo na malalamiko juu ya watuhumiwa kushinda kesi za ubakaji kutokana na ukosefu wa ushahidi wa kutosha.

“Kumekuwepo na tuhuma dhidi ya madaktari ya kuandika maelezo yanayosaidia watuhumiwa wa ubakaji na ulawiti kushinda kesi, lakini jamii inatakiwa ifahamu kwamba daktari huandika maelezo kulingana na hali halisi anayoiona kwa siku hiyo,” amesema na kuongeza;

“Mtoto anapofanyiwa ukatili ni vema jamii ikatoa taarifa mahala husika ndani ya saa 72, pia mhanga asibadilishe nguo alizovaa na wala kuusafisha mwili wake ili kusaidia madaktari kupata vipimo vitakavyothibitisha ukatili huo.”

Mndolwa amesema kuwa, kukithiri kwa maelezo duni sambamba na vithibitisho ndiyo sababu ya watuhumiwa wengi wa ubakaji kushinda kesi mahakamani.

Waziri Nashiri, Mratibu wa Timu ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto Manispaa ya Ilala amesema kuwa, mtoto aliyefanyiwa ukatili akifikishwa kwenye vituo vya afya mapema hupewa dawa zinazozuia maambukizi ya magonjwa hasa wa Virusi vya Ukimwi.

“Lazima muathirika afike katika kituo cha afya ndani ya saa 72, maana tunatoa dawa za kuzuia maambukizi ya magonjwa na ni rahisi kupatikana kwa ushahidi unaokubalika mahakamani na kumtia mtuhumiwa hatiani,” amesema.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya ongezeko la vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika Manispaa ya Ilala, ambapo Tabu Shaibu, Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala anafafanua idadi ya wahanga hao.

“Kuanzia mwaka 2013 Manispaa ya Ilala kupitia kituo cha One Stop Center na Ofisi za Ustawi wa jamii hadi Machi mwaka huu ilipokea watoto 1213 ambao walipatiwa huduma baada ya kufanyiwa vitendo tofauti vya ukatili,” amesema.

“Ongezeko la watoto na wanawake wanaofanyiwa ukatili kwa mfano mwezi Februari mwaka huu watoto 18 walibakwa,na kwa mwezi machi 26 pia walibakwa hii ikiwa ni ongezeko la watoto 8 ndani ya mwezi mmoja na kwamba hwa wote walipelekwa katika kituo cha mkono kwa mkono baada ya kufanyiwa ukatili huo,” amesema Shaibu.

Shaibu amesema kuwa mnamo mwaka 2012 Halmashauri ya Manispaa ya Ilala iliunda timu ya Ulinzi na usalama wa mtotoambayo huratibiwa na Ofisi ya Ustawi wa Jamii chini ya Kitengo cha familia na watoto ambacho imekuwa ikitekeleza majukumu yake katika kuelekea siku ya Mtoto wa Afrika ambayo huazimishwa terehe Juni 16 kila mwaka.

“Timu ya ulinzi imekuwa ikitekeleza mpango kazi wa kitaifa wa kuhudumia watoto walio katika mazingira hatarishi na kusimamia huduma kwa watoto wote kwa kushirikiana na wadau, timu hiyo imesaidia watoto wengi waliokatika mazingira hayo,” amesema.

error: Content is protected !!