Saturday , 22 June 2024
Home Habari Mchanganyiko ALP yazindua ripoti ya soko la Pamoja la Afrika ya Mashariki
Habari Mchanganyiko

ALP yazindua ripoti ya soko la Pamoja la Afrika ya Mashariki

Spread the love

 

KAMPUNI inayojihusisha na usimamizi wa shughuli za kisheria katika nchi za Afrika ya Mashariki, ALP East Africa, imezindua ripoti inayohusu taarifa za soko la Pamoja la Afrika ya Mashariki kuangazia huduma na bidhaa katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo Mkuu wa kampuni ya ALP East Africa, Francis Gimara amebainisha kuwa, “Dhumuni la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ni maingiliano ya ushirikiano wa kiuchumi na maingiliano ya ushirikiano wa kibiashara, ikiwa ni dhumuni la msingi, kama sio la kwanza, la lengo la mchakato wa maingiliano. Maingiliano ya kibiashara ndio msingi wa Mkataba na itifaki za Umoja wa Soko la Pamoja na Forodha, na unatarajiwa kuwa mhimili mkuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.”

“Tukiwa kama watoa huduma zenye maingiliano na ushauri wa kitaalamu wa makampuni ya kisheria kwenye nchi za Uganda, Kenya, Tanzania na Sudani ya Kusini — ALP ni kampuni inayotoa huduma za kisheria na/au ushauri kwenye nchi hizi kwa upande wa biashara pamoja na kuanzisha biashara mpya na usimamizi wake. Msaada wa kiushauri kuhusiana na biashara pamoja shughuli za kibiashara baina ya nchi moja na nyingine ni eneo ambalo ALP East Africa ambalo inalishughulikia mara kwa mara hususani kupitia sheria na tarataibu za kiudhibiti za nchi wanachama wa Afrika ya Mashariki,” aliendelea Gimara.

ALP East Africa inazingatia upitiaji wa Huduma za Soko la Pamoja la Afrika ya Mashariki na kutoa uelewa wa uhusiano kati ya mifumo ya udhibiti wa kitaifa na mfumo wa biashara wa kikanda (Jumuiya ya Afrika Mashariki).

“ALP East Africa inaelewa umuhimu wa wadau katika maeneo ya biashara—katika maoni ya umma, serikali za Jumuiya ya Afrika Mashariki (ikiwa ni pamoja na watendaji wao mbalimbali na wa ngazi tofauti) na, kwa mtazamo binafsi, watendaji wa sekta binafsi (wawekezaji, jumuiya ya wafanyabiashara, na kadhalika,” alimalizia Mkuu huyo.

Kampuni hiyo imetoa ripoti ya Soko la Pamoja la Huduma na Bidhaa za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC CSG Scan) 2022 – 2023 kama sehemu ya usaidizi wake wa ushauri wa kisheria wa mara kwa mara wa kuhusu ushirikiano wa biashara wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Kama hatua ya kwanza, Soko la Pamoja la Bidhaa na Huduma la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC CSG Scan) 2022 – 2023 linatathmini hatua za udhibiti — kulingana na sheria, notisi za kiutawala, maagizo, n.k — zilizochukuliwa na Nchi tano Wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ambazo zinaathiri usafirishaji huru wa mtaji, bidhaa na huduma katika Soko la Pamoja katika kipindi cha Januari mpaka Desemba 2022.

Nchi Wanachama zilizozingatiwa katika uzinduzi na uchunguzi wa awali wa Huduma na Bidhaa za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wa kila mwaka ni Kenya, Rwanda, Tanzania, Sudan Kusini, na Uganda. Mipango iliyopo ni, ALP East Africa inapanga kutoa ripoti ya namna hii kila robo ya mwaka.

Ripoti ya Soko la Pamoja la Huduma na Bidhaa la Jumuiya ya Mashariki (EAC CSG Scan) 2022 – 2023 imezinduliwa kama utangulizi mpana wa ALP East Africa katika Nchi kadhaa Wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na kuzitaka kujikita katika Huduma na Bidhaa za Pamoja chini ya Soko la Pamoja, manufaa yake makubwa kwa hatua za maingiliano ya kibiashara ya Sekretarieti za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Baraza la Sheria la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Baraza la Mawaziri, na taasisi nyingine za Kijumuiya.

Uzinduzi wa Soko la Pamoja la Huduma na Bidhaa za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki 2022 – 2023 ulihudhuriwa na maafisa wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Wajumbe wa Baraza la Sheria la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Asasi za Kiraia, sekta za biashara n.k.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Askofu Wolfang Rais mpya TEC, Padri Kitima aula tena

Spread the loveBARAZA la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetambulisha safu mpya za...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washiriki mbio za NBC Dodoma Marathon kutumia treni ya SGR kwenda Dodoma

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

Habari MchanganyikoTangulizi

Padre anayetuhumiwa mauaji ya Asimwe, asimamishwa

Spread the loveKanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha kutoa huduma za kichungaji...

Habari Mchanganyiko

Upandaji miti uzingatie kuondoa umaskini kwa wananchi

Spread the loveKATIBU Tawala wa mkoa wa Morogoro Dk. Musa Ally Musa...

error: Content is protected !!