January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ally Choki atua rasmi Twanga, kupanda jukwaani Aprili 18

Mkurugenzi wa African Stars, Asha Baraka (kulia) akimpokea mwanamuziki mpya wa bendi hiyo, Ally Chocky muda mchache baada ya kutambulishwa.

Spread the love

HATIMAYE yale maneno ya chinichini yaliyokuwa yanamuhusu mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi, Ally Chocky kuwa atahamia kataika bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ yametimia. Anaandika Erasto Stanslaus … (endelea).

Chocky ametambulishwa rasmi leo kujiunga na bendi ya Twanga Pepeta, katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Nemax Hotel, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mwanamuziki huyo aliyetamba na bendi za Twanga, Double Extra na Extra Bongo, ameliambia MwanaHALISI Online, kuwa ameamua kurejea Twanga Pepeta bila ya kushinikizwa na mtu yoyote bali ni maamuzi yake mwenyewe na hana mpango wa kuihama bendi hiyo tena.

Chocky hakurudi peke yake katika bendi hiyo, ameambatana na dansa wake mahiri ambaye aliondoka naye katika bendi hiyo wakati anaondoka, Super Nyamwela.

Onyesho la kwanza kwa Chocky ndani ya Twanga Pepeta litafanyika tarehe 18 katika ukumbi utakaotajwa hapo baadae, huku mwenyewe akiahidi makubwa kwa mashabiki wa bendi hiyo..

Mwanamuziki huyo amesema ametua katika bendi hiyo na zawadi ya nyimbo tatu ambazo ni ‘Kichwa Chini’, ‘Usiyaogope Maisha’ na ‘No Discussion’.

error: Content is protected !!