Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Aliyetumbuliwa, ateuliwa ubalozi
Habari za Siasa

Aliyetumbuliwa, ateuliwa ubalozi

Spread the love

DAKTARI Modestus Kipilimba, aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), ameteuliwa kuwa balozi. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Rais Magufuli alimfuta kazi Dk. Kipilimba tarehe 12 Septemba 2019, ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Diwani Athumani, aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Kwa niaba ya Rais John Magufuli, uteuzi huo umetangazwa na Balozi John Kijazi, Katibu Mkuu Kiongozi leo tarehe 20 Septemba 2019.

Balozi Kijazi amesema, kituo cha kazi cha Dk. Kipilimba kitatangazwa hapo baadaye.

Wakati huo huo, Balozi Kijazi amesema, Rais Magufuli ameteua mabalozi wapya 12 watakaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi kuziba nafasi zilizo wazi kufuatia wengine kumaliza muda wao, kustaafu na kurejeshwa nyumbani.

Wateule hao wa ubalozi ni pamoja na Mohamed Mtonga, Dk. Jilly Maleko, Dk. Benson Bana, Meja Jen. (Mst), Anselimu Bahati, Prof. Emmanuel Mbennah na Maimuna Tarishi.

Wengine ni Meja Jen. (Mst) Gaudence Milanzi, Ali Jabir Mwadini, Jestas Nyamanga, Dr. Kennedy Gastorn, Mhandisi Aisha Amour.

Balozi Kijazi ametaja vituo vitakavyojazwa na mabalozi wapya ambavyo ni Falme za Kiarabu (Abu Dhabi), Burundi, Ubelgiji, Misri, Zimbabwe, Kuwait, Afrika Kusini, Saudi Arabia (Riyal).

Vituo vingine ni Japan, Umoja wa Mataifa (Switzerland), Umoja wa Mataifa (New York) na Nigeria.

Pia, Balozi Kijazi amesema, Rais Magufuli amemteua Mwenyekiti wa CCM mkoani Arusha,  Lowata Sanare kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akichukua nafasi ya Stephen Kebwe ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Balozi Kijazi amesema, Rais Magufuli amefanya mabadiliko ambapo, amemhamisha Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Charles Kabeho kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato.

Balozi Kijazi amesema, nafasi ya Kabeho imechukuliwa na Msafiri Mtemi, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato.

Katika mabadiliko hayo, Balozi Kijazi amesema Rais Magufuli amemteua Musa Masele kuwa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

error: Content is protected !!