August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Aliyesuka njama kumuua balozi wa Urusi atajwa

Spread the love

FETHULLAH Gulen Kiongozi wa Dini ya Kiislamu anayeishi uhamishoni nchini marekani ametajwa kuhusika katika njama za kumuua Andrey Karlov Balozi wa Urusi nchini Uturuki tarehe 19 Desemba mwaka huu. anaandika Wolfram Mwalongo.

Recep Tayyip Erdogan, Rais wa Uturuki ametoa taarifa kuwa kijana aliyehusika kutekeleza shambulizi hilo mwenye umri wa miaka 22 ni mtu wa karibu wa Gulen.

Hata hivyo Urusi imeyapuuza madai hayo kutokana na Rais Erdogan kuwafungasha virago watu wote waliokuwa wakimuunga mkono kiongozi huyo wa kiislamu.

Makachero wa Urusi (FSB), waliwasili jijini Ankara Desemba 20 kwa ajili ya kufanya uchunguzi ili kubaini wahusika waliohusika na kifo cha balozi huyo.

Balozi Andrey Karlov aliuawa wakati akiwa kwenye jumba la maonesho ya picha (sanaa), alipigwa risasi mgongoni na kijana aliyeonekana kuwa na jazba,Ingawa kijana huyo ametajwa kuwa askari wa uturuki.

Fethullah Gulen amekuwa kuwa adui mkubwa wa Serikali ya Uturuki katika kipindi hiki hususan baada ya kutajwa kuhusika na jaribio la mapinduzi ya Serikali Uturuki Julai 15 mwaka huu, madai ambayo Gulen amekuwa akikanusha.

Hata hivyo Marekani imetajwa kumkingia kifua kwakile kinachodaiwa ni raia wake lakini pia ikisema uthibitisho unaotolewa na Uturuki ili kumchukulia hatua kiongozi huyo hauna mashiko, jambo ambalo linachochea kuzorotesha mahusiano ya mataifa haya mawili.

error: Content is protected !!