July 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Aliyemwita Magufuli ‘Bwege’ ahukumiwa

Spread the love

ISAAC Abakuki, aliyetuhumiwa kumwita Rais John Magufuli ‘bwege’ amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu au kulipa Sh. 7 milioni, anaandika Wolfram Mwalongo.

Fedha hizo anatakiwa kulipa kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza anatakiwa kulipa mwezi Julai Sh. 3.5 milioni na mwezi Agosti anatakiwa kulipa Sh. 3.5 milioni.

Hukumu hiyo imetolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na Augustine Rwizile, Hakimu wa mahakama hiyo.

Abakuki alishitakiwa kwa madai ya kumkashifu Rais Magufuli katika ukurasa wake wa Facebook.

Hata hivyo, alikiri kutenda kosa hilo tarehe 17 Machi ambapo akiwa nyumbani kwake Olasiti, Arusha alioa ujumbe kwenye akaunti yake ya Facebook ukisema ‘mnamlinganishaje Magufuli na Nyerere’  uliokuwa umeanzishwa na Kituo cha Clouds.

Hata hivyo, baada ya kuona ujumbe alijibu  ‘Hizi ni siasa za maigizo halafu mnamfananisha huyu bwege na Nyerere, wapi  buana?”

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilianza kumfuatilia na baadaye kukamatwa na kufikshwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

 

error: Content is protected !!