August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Aliyemuweka’ Mtanzania rehani kizimbani

Spread the love

JUMA Mwinyi, mkazi wa Dar es Salaam amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kumuweka nduguye rehani nchini Pakistani, anaandika Faki Sosi.

Mwinyi anadaiwa kumweka ndugu yake Adam Akida nchini Pakistan kama dhamana baada ya kuchukua mzigo wa dawa za kulevya.

Hatua hiyo imefikiwa ikiwa ni mwezi mmoja sasa baadhi ya mitandao ya kijamii pia gazeti moja la kila siku kuripoti taarifa za Akida kuteswa na watu wanaotajwa kuwa wauzaji wa wakubwa wa dawa za kulevya Pakistan kumshikilia wakisisubiria malipo yao.

https://www.youtube.com/watch?v=7mMa979_KLY

Kumekuwepo na taarifa za Adam kuwekwa reheni na ndugu yake ambaye alipokea mzigo wa dawa za kulevya kwa ahadi ya kuuza na kulipa thamani ya mzigo huo kisha kumchukua ndugu yake.

Leo katika Mahakama ya Kisutu Juma amefunguliwa mashitaka ya kufanya biashara ya kisafirisha binaadamu pamoja na kumweka kijana huyo rehani.

Akisoma mashtaka hayo Peter Njike, mwendesha mashitaka wa serikali mbele ya Cyprian Mkeha, Hakimu Mfawidhi katika mahakama hiyo amedai kuwa, mtuhumiwa huyo anadaiwa kufanya biashara hiyo.

Amedai, kati ya mwezi Desemba 2015 na Januari 2016  alimsafirisha Mtanzania anayefahamika kwa jina la Adam Akida kwenda nchini Pakistan.

Mshitakiwa amekana mashtaka hayo ambapo upande wa Jamhuri umesema kuwa, upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.

Hakimu Mkeha amesema kuwa, shauri hilo halina dhamana na kwamba, kesi hiyo itatajwa tena tarehe 17 Agosti mwaka huu.

error: Content is protected !!