July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Aliyelawiti watoto atiwa mbaroni

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Morogoro, linamshikilia Alhaji Dotto (27) mkazi wa Sabasaba Manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za kuwalawiti watoto wawili, anaandika Christina Haule.

Leonce Rwegasira, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro amesema, tukio hilo limetokea tarehe 13 Agosti mwaka huu, saa 5:00 usiku katika maeneo ya uwanja wa Taifa, Manispaa ya Morogoro.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwalawiti watoto wawili ambapo mtoto wa kwanza, ana umri wa miaka (03) na mwingine ana umri wa miaka (05).

“Tukio hili liligunduliwa na Zainab Abdul (27) mkazi wa uwanja wa Taifa ambaye ni mama wa mtoto mwenye umri wa miaka mitatu ambapo mtoto huyo alilalamika kusikia maumivu makali sehemu zake za siri pamoja na mtoto wa jirani yake mwenye miaka mitano,” amesema Kamanda Leonce na kuongeza;

“Baada ya mwanamke huyo kuwadadisi watoto hao ndipo walipomtaja mtuhumiwa huyo kuwa ndiye aliyewatendea kitendo hicho na kisha Jeshi la Polisi tukamkamta kwa mahojiano zaidi na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.”

Watoto hao wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

error: Content is protected !!