Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Aliyekuwa mgombea udiwani NCCR-Mageuzi atimkia Chadema
Habari za Siasa

Aliyekuwa mgombea udiwani NCCR-Mageuzi atimkia Chadema

Frank Rugwana
Spread the love

ALIYEKUWA mgombea Udiwani wa Saranga Jimbo la Kibamba, Dar es Salaam kupitia NCCR-Mageuzi, Frank Rugwana ametangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Rugwana, alikuwa mgombea kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita ambao ulifanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

Rugwana amechukua uamuzi huo leo Jumamosi tarehe 23 Januari 2020 katika ofisi ya Chadema jimbo la Kibamba iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kukabidhiwa kadi ya uanachama wa Chadema na aliyekuwa mgombea ubunge wa Kibamba kupitia Chadema, Ernest Mgawe, Rugwana alizungumza kwa kifupi mbele ya waandishi wa habari kueleza dhamira yake.

“Nimeona nijiunga na Chadema, chama ambacho kinauwezo wa kupambana na demokraisa na nimejiunga na Chadema ili kuendeleza mapambano.”

Lakini mapambano na maono ya mtu hayawezi kutimia kama utaunga juhudi au kupindisha ukweli na hata kujipendekeza ili uweze kuteuliwa, hili halikubaliki,” amesema Rugwana

Amesema, yeye kama mwanasiasa na kwa akili zake timamu amelitafakari kiundani suala la kujiunga na chama hicho na sababu kubwa ilimpekekea kuhamia huko ni baada ya kubaini ndio chama kikubwa chenye nguvu.

“Nimeona chama kikubwa cha upinzani chenye nguvu na ushawishi mkubwa ni Chadema. Nimejiunga nikiwa na akili zangu timamu ili niendeleze mapambano ambayo wenzetu wanayafanya, naomba ushirikiano wenu,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!