January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Aliyekuwa Meya Bukoba aachiwa

Meya wa Manispaa ya Bukoba, Dk. Anatory Amani

Spread the love

DAKTA Anatory Amani-Meya aliyeng’olewa kuiongoza Halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera mwaka jana, kutokana na kuendesha miradi ya kifisadi, leo ameachiwa na Jeshi la Polisi baada ya kushikiliwa kwa siku tatu kwa kosa la upotevu wa silaha yake. Anaandika Mwandishi Wetu, Bukoba …(endelea).

Mwanasiasa huyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kagondo, alishikiliwa katika Kituo cha Polisi Bukoba kutokana na upotevu wa silaha anayoimiliki-bastola aina ya Browning pamoja na risasi nane, ambayo kisheria alitakiwa kuikabidhi polisi alipokuwa safari.

Hatua hiyo, ilitokana na Dk. Amani kuripoti kituoni hapo juzi saa nne usiku kupotelewa na silaha hiyo nyumbani kwake wakati akiwa safarini nchini Burundi tangu Machi 27 mwaka huu.

Taarifa zilizopatikana zinasema kuwa, Dk. Amani ameachiwa baada ya silaha hiyo kupatikana mkoani Geita ikiwa mikononi mwa mjukuu wake aliyekuwa akimtuhumu kuiiba. Kwa sasa mtuhumiwa huyo yuko ndani akiendelea na mahojiano.

Awali ilidaiwa kuwa kushikiliwa kwa Dk. Amani kulitokana na kutajwa kufadhili matukio ya kushambulia na kuwakata watu makoromeo, vitendo ambayo vinazidi kushika kasi wilayani Bukoba.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe, alifafanua kushikiliwa kwa Dk. Amani, akisema alitenda kosa la ukiuwaji wa usimamizi wa silaha ambayo alifika kituoni kuripoti kwamba iliibiwa baada ya nyumba yake kuvunjwa.

Mwaibambe amesema Dk. Amani alieleza kuwa aliposafiri alimwachia sialaha mjukuu wake wa kidato cha pili nyumbani kwake, lakini aliporudi hakumkuta, isipokuwa alikuta nyumba imevunjwa huku kompyuta yake mpakato aina ya Dell na silaha yenye risasi nane havikuwepo.

error: Content is protected !!