September 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Aliyekataa U-DC, akubaliwa

Spread the love

HATIMAYE Dk. John Magufuli, Rais wa Tanzania amesikia kilio cha Ally Masoud Maswanya, aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mbeya cha kuomba uteuzi wake utenguliwe kutokana na sababu binafsi, anaandika Hamisi Mguta.

Maswanya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo tarehe 26 Juni mwaka huu wakati Rais Magufuli alipotangaza wakuu wa wilaya 139 na baadaye kuomba atenguliwe kutokana na sababu binafsi kama alivyoeleza.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu inaeleza kuwa, Rais Magufuli leo amemuhamisha John Ernest Palingo aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Songwe mkoani Dodoma kuwa, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi.

Wakati huo huo rais amemteua Deogratius John Ndejembi kuwa Mkuu wa wilaya wa Songwa Mkoani Dodoma kuchukua nafasi ya Mh. Palingo.

“Uhamisho huo umefanywa baada ya rais kuridhia maombi ya Bw. Ally Masoud Maswanya aliyeteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Mbozi kuomba uteuzi wake utenguliwe kutokana na sababu binafsi,” imeeleza taarifa.

Ngejembi atakula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma 12 Julai mwaka huu Ikulu Jijini Dar es Salaam.

 

error: Content is protected !!