Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Aliyekaa nusu karne bila kuoga afariki baada ya kuoga
Kimataifa

Aliyekaa nusu karne bila kuoga afariki baada ya kuoga

Amou Haji
Spread the love

 

MTU mchafu zaidi duniani Amou Haji aliyekaa zaidi ya miaka 50 bila kuoga amefariki duniani miezi michache baada ya kuogeshwa kwa lazima. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Haji alikuwa amekataa kutumia sabuni na maji kwa zaidi ya nusu karne, akihofia ingemfanya kuwa mgonjwa.

Raia huyo wa Iran , ambaye aliishi katika jimbo la kusini la Fars, aliepuka majaribio ya hapo awali ya wanakijiji kutaka kumsafisha.

Lakini, kulingana na vyombo vya habari vya ndani, Haji hatimaye alikubali shinikizo na kuoga miezi michache iliyopita.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA la Iran, aliugua muda mfupi baadaye na kufariki siku ya Jumapili.

Katika mahojiano ya awali, yaliyotolewa na gazeti la Tehran Times mwaka 2014, Haji alifichua chakula anachopenda zaidi ni nungu, na kwamba aliishi kati ya shimo ardhini na kibanda cha matofali kilichojengwa na wakaazi wa kijiji cha Dejgah.

Amou Haji

Aliiambia kituo hicho kwamba uamuzi wake ulitokana na vikwazo vya kihisia wakati alipokuwa mtoto mdogo.

Kutooga kwa miaka mingi kulimwacha akiwa ngozi yake imezibwa na tope na usaa, IRNA ilisema, huku chakula chake kikiwa nyama iliooza na maji chafu .

Haji hakujulikana kuwa na familia , lakini wanakijiji walijaribu kumuangalia.

Pia alikuwa akipenda kuvuta sigara, akipigwa picha angalau mara moja akivuta sigara zaidi ya mara moja.

Jaribio la kumuogesha, au kumpa maji safi ya kunywa, lilimhuzunisha, shirika hilo la habari lilisema.

Hata hivyo, iwapo anashikilia rekodi ya kukaa muda mrefu zaidi bila kuoga limekuwa suala la mjadala.

Mnamo 2009, kulikuwa na ripoti za mwanamume wa India ambaye – wakati huo – hakuosha au kupiga mswaki kwa miaka 35.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

Habari MchanganyikoKimataifa

Wanafunzi 130 waliokuwa wametekwa nyara waokolewa

Spread the loveZaidi ya wanafunzi 130 wa shule ya msingi LEA na...

Habari MchanganyikoKimataifa

Mgombea upinzani aongoza uchaguzi wa Rais Senegal

Spread the loveMgombea wa upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye ameonekana kuongoza...

error: Content is protected !!