Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Aliyeibiwa mtoto kuwaponza madaktari
Habari Mchanganyiko

Aliyeibiwa mtoto kuwaponza madaktari

Spread the love

ILIKUWA ni mwanzoni mwa Aprili mwaka 2017 ambapo taarifa za Asma Juma, kuibiwa mtoto katika Hospitali ya rufaa ya Temeke ziliposambaa, anaandika Hamisi Mguta.

Mwanamke huyo alifika hospitalini hapo kujifungua, lakini alidai kuwa ameibiwa mtoto wake baada ya kujifungua mapacha na kukabidhiwa mtoto mmoja tu badala ya wawili.

Prof. Charles Majinge, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi iliyoundwa kuchunguza suala hilo, amewasilisha ripoti yake kwa Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeeleza kuwa Asma hakuwa na ujauzito wa mapacha kama ilivyodaiwa.

“Kamati imebaini na kujiridhisha kuwa alikuwa na ujauzito wa mtoto mmoja na ukuaji wa tumbo ulikuwa ni wa kawaida na wapimaji wote waliopima walipata matokeo ya kukinzana na madai ya kuwepo kwa ujauzito wa watoto wawili.

“Hata wakati wa kujifungua ilionekana akijifungua mtoto mmoja mbele ya mashahidi sita,” amesema.

Katika hatua nyingine, waziri Ummy ameagiza madaktari waliomuhudumia mwanamke huyo bila kumpima kwa vipimo vya Ultrasound washughulikiwe.

“Namuandikia George Simbachawene, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kumuelekeza Katibu Mkuu wa Tamisemi awashughulikie madaktari ambao hawakutekeleza wajibu wao.

“Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, mgonjwa anaenda na vipimo vyake vya Ultrasound wakati vipimo vipo palepale, walishindwa kitu gani kumfanyia vipimo kuhakikisha kama ana ujauzito wa mapacha au au la,” amesema Ummy.

Hapo awali, Asma alieleza kuwa alikuwa akipata huduma za kliniki katika Zahanati ya Serikali ya Mbande, na alifanya vipimo vya picha maarufu kama Ultrasound katika Zahanati binafsi ya Huruma iliyopo Mbande mara mbili na kupewa majibu kuwa ana ujauzito wa mapacha.

Alipokuwa akitoa madai yake Asma alisema, “Wakati napelekwa chumba cha upasuaji nilikuwa sina kichaa cha uzazi, siumwi uchungu, siumwi kichwa, siyo kipofu, siyo kiziwi, nina kumbukumbu zote. Ninachotaka ni mtoto wangu.”

Hata hivyo, Jordan Massive, mwakilishi wa familia ya Asma siku ya leo amewambia wanahabari kuwa wameyapokea matokeo hayo kutoka kamati ya uchunguzi bila hiyana.

“Ningependa kuvishukuru vyombo vya habari kwasababu ndivyo vilivyoibua sakata hili na kwa niaba ya familia nashukuru kwa kuweza kufikia tamati ya tatizo hili.

“Bado tupo kwenye mchakato wa kumuweka sawa Asma kisaikolojia kwani tangu kutokea kwa tukio hilo hayupo sawa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!