Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Aliyefariki kwenye foleni ya mbolea azua zogo bungeni
Habari za SiasaTangulizi

Aliyefariki kwenye foleni ya mbolea azua zogo bungeni

Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson
Spread the love

 

TAARIFA za mwananchi aliyedaiwa kupoteza maisha akiwa kwenye foleni ya mbolea wilayani Songea mkoani Ruvuma, zimeibua mvutano mkali bungeni baada ya Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Kunti Yusuph Majala kuhusianisha tukio hilo na changamoto ya upatikanaji wa pembejeo kwa wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akichangia mjadala kuhusu ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) leo tarehe 5 Novemba, 2022 bungeni jijini Dodoma, Majala ameishauri Serikali kusogeza huduma hiyo ya ugawaji wa mbole ya ruzuku katika makao makuu ya Kata badala ya wilayani ili kupunguza umbali kwa wananchi kufuata huduma hiyo.

“Jana wakati naangalia taarifa ya habari kuna mwananchi mmoja Songea amefariki akiwa kwenye foleni anasubiri mbolea…kapanga foleni ameanguka chini na kufariki kutokana na msongamano wa kwenda kutafuta mbolea.

“Tunachokuomba waziri (Hussein Bashe) hao mawakala wako ambao wanasambaza mbolea uliowapa hiyo kazi tunaomba mbolea hii isikae makao makuu ya wilaya ama kwenye hivyo vituo, tuende angalalu tuwasogezee makao makuu ya kata ambako kwanza tutapunguza hiyo foleni lakini tutawapunguzia wananchi kazi ya kutembea umbali mrefu kufuata hiyo mbolea,” amesema.

Wakati akitoa mchango huo, Mbunge wa Nyang’wale, Hussein Amar (CCM) alisimama na kutoa taarifa kwa Majala kwamba kufariki kwa mwananchi akiwa kwenye foleni akisubiri mbolea hiyo ni ahadi ya Mwenyezi Mungu wala sio sababu ya mbolea.

Hata hivyo, Majala alikataa taarifa hiyo na kudai kuwa ingekuwa ni ahadi ya Mungu angefia huko nyumbani kwake.

“Lakini laiti isingekuwepo foleni na tunafahamu watanzania wengi hatuna utamaduni wa kucheck afya zetu hata kama alikuwa na maradhi yake katika mazingira hayo chanzo kilichoripotiwa ni mkulima kufariki kwenye foleni akitafuta mbolea,” amesema.

Naye Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel na kutoa taarifa kuwa sababu za vifo haziamuliwa na taarifa za magazeti na kwamba mtu anaweza kufariki akitembea.

“Inawezekana mbunge anataka kuonesha uzito ila sababu sio kukaa kwenye foleni ya mbolea,” alitoa taarifa kwa Majala.

Aidha, Majala alisisitiza hakuna sababu ya kuvutana ila suala la msingi ni mtu amefikwa na umauti akisubiri mbolea.

Mwanasheria Mkuu wa serikali, Dk. Eliezer Feleshi naye alisimama kutoa taarifa kwamba kwa mujibu wa kanuni ya 71 1(a), wabunge hawapaswi kutoa taarifa ambazo hazina ukweli.

Dk. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya

Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson alimhoji Dk. Feleshi kwamba ni taarifa gani haina ukweli, ambapo mwanasheria hiyo alifafanua kuwa kifo cha binadamu hudhibitishwa na daktari.

Ameongeza mchango wake mbunge una taarifa za upande mmoja ambayo haiwezi kutolewa kwenye mamlaka na kufanyiwa kazi.

Hata hivyo, Spika Tulia alihitimisha mvutano huo kwamba Majala ametumia taarifa huyo kuelezea changamoto ya upatikanaji wa huduma hasa ikizingatiwa taarifa za CAG zinaonesha kuna upotevu wa mapato.

“Mtu ni kweli amefariki na huyo mtu amefariki akiwa kwenye eneo ambalo linatolewa mbolea, ikiwa hilo silo linalobishaniwa ina maana Majala yupo sawa na mimi katika kusikiliza sijasikia akisema kilichosababisha kifo ni foleni ya mnbolea, anaelezea amefia kwenye eneo la kusubiri mbolea.

“Kama huyo mtu hajafa hilo ni suala lingine, kama hajafia pale kwenye eneo la mbolea inapotolewa hilo ndilo linaweza kubishaniwa pia ila mtu amefariki kwenye eneo la kusubiri mbolea hilo sio la kubishaniwa,” alihitimisha Spika Tulia na kutoa nafasi kwa Majala kuendelea na mchango wake.

Hata hivyo, Majala alihitimisha mchango wake kwa madai kuwa akiendelea ataharibu zaidi hali ya hewa. Ila ametoa wito kwa wabunge kusikiliza na kutafakari ili kuchukua maamuzi badala ya kutetea na kubebana katika mambo yasiyokuwa na tija.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!