Thursday , 7 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Aliyedai kudhurumiwa shamba amvaa Lukuvi bungeni
Habari za Siasa

Aliyedai kudhurumiwa shamba amvaa Lukuvi bungeni

Spread the love

MKAZI wa kijiji cha Nyahanga, Wilayani Kahama, Shinyanga, Magohe Kafumu, amemfuata bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, ili amsaidie kupata haki yake ya ardhi hekari 20 alizonyang’anywa na baraza la ardhi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kafumu alisema lengo lake ni kuhakikisha kuwa anamfikishia kilio chake Waziri huyo kutokana na kukosa msaada katika wilaya yake.

Alisema amehangaika kwa muda mrefu kupata msaada katika ngazi tofauti bila mafanikio, sasa ameamua kufunga safari na kuja jijini Dodoma ilia pate fursa ya kuonana na Waziri Lukuvi.

Alisema eneo analolilalamikia ni la ukubwa wa hekari 20, ambalo alinunua kwa Ilagila Kapagala kwa Sh. 3.5 milioni mwaka 2013.

Alisema kabla ya kulinunua eneo hilo alikuwa akikodi kwa mwaka kwa gharama ya Sh. 200,000 lakini baadaye mmliki wa eneo hilo akadai kumuuzia.

“Aliposema kuwa anauza nikamuuliza shilingi ngapi akasema kwa sababu nimekuwa nakodi basi impatie shilingi 3,5 milioni, nikaanza kumpatia kwanza milioni moja, baadaye mkewe akafuata nyingine na tulikuwa tukiandikisha kwa mwenyekiti wa kijiji na nakara zote zipo,” alisema. 

Aidha mara baada ya kulinunua na kuanza kulima alipata Samansi kutoka baraza la ardhi la wilaya ya Kahama alipokwenda aliiambiwa hatakiwi kufanya chochote kile katika eneo hilo ambalo tayari alisha lima mpunga na kutumia gharama kiasi cha Sh. milioni 17,350,000.

Alifafanua kuwa jambo la kushangaza ni namna ambavyo kesi hiyo ilienda kwani katika siku zote za kuhudhuria vikao vya baraza hilo mlalamikaji hakuwahi kufika hata siku moja wala mashahidi hawakuitwa kutoa ushahidi wao.

“Hukumu wakatoa wao kuwa natakiwa kuliachia shamba na mpaka mwezi juni mwaka huu natakiwa kutoa vitu vyangu lakini kinachonekana hapa ni kuna watu wanalitaka eneo lile tena kwa bei ya juu na ni viongozi wakubwa wa wilaya yetu,” alisema Kafumu.

Akizungumza kwa njia ya simu aliyekuwa Mwenyekiti wa kijiji cha Nyahanga, Daudi Samsoni alisema katika Uongozi wake alishuhudia sehemu ya mauziano ya eneo hilo na kudai kuwa ushahidi wote anao.

“Mimi nikiwa kiongozi sehemu ya mauziano nilishiriki kama mwenyekiti lakini nashangaa kwanini sisi kama mashahidi hatujaitwa na mlalamikaji hakuwahi kwenda katika kesi lakini maamuzi yametolewa”alisema Samsoni.

Akijibu malalamiko hayo Mwenyekiti wa baraza la ardhi Wilaya ya Kahama, Paulo Lekamoy, alisema kama kuna mtu anaona kuwa haki haikutendeka akate rufaa au aende kokote anakoona kutamsaidia.

“Kama amekuja hapo na anadai anataka kwenda kwa waziri mwache aende na kama hajaridhika na maamuzi basi akate rufaa sina maneneo mengine ya kusema nina kazi nyingi za kufanya,” alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

error: Content is protected !!