Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Michezo Alikiba: Mfalme ni mmoja tu, albam wiki ijayo
Michezo

Alikiba: Mfalme ni mmoja tu, albam wiki ijayo

Ali Kiba
Spread the love

 

HATIMAYE Staa wa Bongofleva nchini, Ali Salehe Kiba maarufu kama Alikiba ametangaza kuachia albam yake ya tatu inayokwenda kwa jina la ‘The Only King. Anaripoti Matilda Buguye na Patricia Kighono, TUDARCo … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 29 Septemba 2021 jijini Dar es Salaam, Alikiba amesema albam hiyo ataiachia tarehe 7 Oktoba mwaka huu.

Amesema albam hiyo yenye nyimbo 16, amechagua kuipa jina hilo la The Only King kwani ndilo jina linaloendana na hisia za mashabiki wake na nafasi yake kwenye Bongofleva.

Pia ameongeza kuwa amechagua jina hilo kwa sababu mfalme ni moja tu na hakuna wafalme wawili kwa maana hiyo yeye atabaki kuwa mfalme kwenye Bongo fleva ambayo amedumu kwa muda wa miaka 19 mfululizo.

Aidha, Kiba amesema ndani ya albam hiyo ameshirikisha wasanii mbalimbali kutoka Barani Afrika.

“Albam hii ilihitaji maandalizi makubwa ndio maana nilichelewa kuitoa licha ya kuitambulisha kwa muda mrefu.

“Lebo yetu ya Kings music imeshirikiana na Ziik ambayo ni kampuni ya kuuza muziki katika kuandaa albam hiii hivyo mashabiki wangu watarajie mambo makubwa,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!