October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Alhaj Mwinyi mwenyekiti mpya MUHAS

Rais John Magufuli na Rais Ali Hassan Mwinyi

Spread the love

RAIS John Magufuli amemteua Alhaji Ali Hassan Mwinyi,  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo tarehe 25 Septemba 2019 na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Msigwa, Alhaji Mwinyi ameteuliwa kuendelea kuwa Mkuu wa chuo cha MUHAS kuanzia leo.

Wakati huo huo, taarifa ya Msigwa inaeleza kwamba Rais Magufuli amefanya uteuzi wa wenyeviti wanne wa bodi za taasisi mbalimbali.

Rais Magufuli amemteua Prof. Mayunga Nkunya, aliyewahi kuwa Katibu wa Baraza la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (IUCEA) kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), akichukua nafasi ya Profesa Jacob Mtabaji ambaye muda wake umemalizika.

Prof. Idrissa Mshoro, ameteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA). Kabla ya uteuzi huo,  Prof. Mshoro alikuwa Profesa wa Uhandisi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Rais Magufuli amemteua Prof. Elias Bisanda kuendelea  kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Prof. Apollinaria Pereka ameteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) akishika nafasi hiyo kwa kipindi cha pili.

Taarifa ya Msigwa imeeleza kuwa, uteuzi wa wenyeviti hao unaanza leo tarehe 25 Septemba 2019.

error: Content is protected !!