Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari Algeria yampa somo Kim Poulsen, alia na uzoefu
Habari

Algeria yampa somo Kim Poulsen, alia na uzoefu

Kim Poulsen Kocha wa Taifa Stars
Spread the love

 

BAADA ya kupoteza kwa mabao 2-0, dhidi ya Timu ya Taifa ya Algeria, kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Kim Poulsen amekili mechi hiyo kumpa funzo kuelekea michezo ijayo, huku akisifu ubora wa wapinzani wake. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa kundi F, wakufuzu kwa fainali za michuani ya kombe la Mataifa Afrika (AFCON) ulipigwa jana Juni 8 mwaka huu, majira ya saa 1 usiku kwenye dimba la Benjamin Mkapa.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Kim alisema kuwa walichojifunza kwenye mchezo huo dhidi ya timu kubwa, ni kutofanya makossa kwani wanauwezo wa kukuadhibu.

“Tulichojifunza leo Unapocheza na timu kubwa, makosa madogo yanakufanya uadhibiwe, tulijaribu kuwashambulia kipindi cha pili mara nyingi kwa kutengeneza nafasi lakini kwenye dakika za mwisho walifanikiwa kumaliza mchezo kwa kupata bao.” Alisema Kim

Huu ni mchezo wa pili kwa Stars, katika kampeni yao, huku mpaka sasa ikiwa haijaondoka na ushindi wa aina yoyote katika michezo miwili ya mwanzoni.

Aidha kocha huyo aliendelea kufunguka kuwa, licha ya kupoteza mchezo huo, lakini kiwango walichokionesha kitawasaidia kwenye michezo ijayo.

“Niliwaambia wachezaji wangu, kiwango hiki kimetuangusha leo, lakini lazima mujue kwamba kiwango cha leo ndio kinatupa muendelezo Zaidi katika kuelekea mchezo ujao mwezi septemba.” Alisisitiza Kim

Matokeo hayo yanafanya Stars, kuwa na alama moja na kushika mkia kwenye F, mara baada ya kucheza michezo miwili.

Kim hakuishia hapo tu, bali aliendelea kusema kuwa kwenye kila mchezo anajaribu kujifunza kitu, huku akisisitiza wachezaji wa Stars wanapawa kuwa na ubora kama walivyo Algeria.

“Kila mchezo tunaocheza unanipa maswali na majibu, kwa mfano leo nimepata swali ya kuwa kifupi wachezaji wetu wanakuwa na ubora na haraka kama waivyo wa Algeria.”

“Kwa kujifunza nimejifunza kwamba lazima tuwe na uzoefu na sio tu kwa njia ya kujifunza” Alisema kocha huyo

Mara baada ya mchezo huo, Stars itamenyana na Uganda kwenye mchezo ujao ambao utapigwa mwezi septemba mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!